LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAWAWA APONGEZA UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA KWA AMANI WILAYANI KAHAMA.

Na:Shaban Njia;Kahama
SERIKALI Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imewashukuru Wananchi pamoja na Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini kwa kuweza kufanikisha uchaguzi wa Rais, Wabunge, pamoja na Madiwani kumalizika kwa amani bila ya kuwa na kasoro yeyote Wilayani hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Waandishi wa habari Ofisin Kwake ambapo alisema kuwa anashukuru Wananchi wa Majimbo matatu yote ya Uchaguzi katika Wilaya ya Kahama kufanya uchaguzi huo kwa amani ingawa kulikuwa na kasoro ndogondogo

Kawawa aliendelea kusema kuwa anashukuruku pia vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama vilivyoshirikia katika kuhakikisha kuwa kunakuwa na hali ya utulivu hali ambayo ilichangia kiasi kikubwa katika kufanikisha zoezi hilo bila ya kuwa malalamiko yeyote.

“Hata ninyi Waandishi wa habari ninatambua mchango wenu mlioutoa katika kuhakikisha kuwa mnatoa habari za kweli bilaya ya kupendelea chama chochote hali iliyochangia pia kuwa na amani na utulivu katika zoezi hilo la uchaguzi”, Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Alisema kuwa baadhi ya Maeneo ambayo yalionekana kuwa makorofi kama vile kata  za Bugarama, Bulyanhulu pamoja na Majengo  tuliamua kupeleka polisi kwa ajili ya kulinda amani na sii kuwabugudhi Wananchi na kuongeza kuwa zoezi hilo liliweza kufanikiwa kwa asilimia 100.

Hata hivyo katika Uchaguzi huo Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa kuna baadhi ya kundi la watui wachache walijaribu kuvuruga uchaguzi huo lakini walidhibitiwa na kuongeza kuwa kundi kubwa la Wananchi walipiga kura kwa amani na utulivu.

Kawawa akizungumzia kuhusu viongozi wa Madhehebu ya kidini alisema kuwa alikaa nao kabla ya uchaguzi na kuwaomba Watoe ujumbe kwa waumini wao kufanya Ibadala mapema ikiwezekana siku moja kbala ya uchaguzi na zoezi hilo lilifanikiwa kiasi kibuwa.

“Nilikaa na Viongozi wa Dini zote na kuwaeleza juu ya kutoa ujumbe kwa waumini wao kufanya Ibada mapema ili Wananchi waweze kuwahi katika zoezi la kupiga kura za kumchagua Rais atakayetuongoza kwa kipindiu cha mika mitano ijayo ikiwa ni sambamba na Wabunge na Madiwani”, Alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.

Katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015 katika Wilaya ya Kahama yenye majimbo matatu ya Uchaguzi ilishudia Aliyekuwa Mbunge wa Msalala Ezekiel Maige akiweza kutete jimbo lake, Eliasi Kwandikwa akishinda katika jimbo la Ushetu pamoja na Jumanne Kishimba aliyeweza kushinda aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama James Lembel katika Jimbo la Kahama Mjini.

No comments:

Powered by Blogger.