KISHIMBA ASEMA BUNGE LIJALO LITAKUWA NA WABUNGE WA DARASA LA SABA LAKINI WENYE KUTIMIZA WAJIBU WAO.
Na:Shaban Njia; Kahama
Mbunge Mteule wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba (CCM) amesema kuwa kwa mara ya kwanza bunge la Jumuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo litashuhudiwa likiwa na baadhi wabunge wenye elimu ya darasa la saba lakini wenye kutimiza majukumu yao vyema.
Kishimba aliyasema hayo juzi katika hafla ya kutathimini hali ya uchaguzi ya Uraisi, Wabunge na Madiwani katika Majimbo matatu ya Uchaguzi ya Kahama Mjini, Ushetu pamoja na Msalala iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa.
Alisema hayo kufuatia baadhi ya watu kumbeza ya kuwa elimu yake ni ya darasa la saba na hatakuwa na uwezo wa kuwawakilisha wananchi wa Jimbo la Kahama Mjini.
“Mimi nimezunguka nchi nchi nyingi Duniani na nimekaa na watu wenye elimu kubwa na kujifunza mambo mengi sana, na nimwekeza biashara zangu ndani na nje ya nje ikiwemo Zimbawe na China ambapo kupitia biasahara hizo nimeweza kujifunza elimu ya maisha na ya kibiashara ambayo itanisaidia kumudu majukumu yangu vyema”. Alisema Kishimba.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa aliwakumbusha wagombea wote kuwa na utamaduni wa kurejea katika majimbo yao pindi vikao vya bunge vinapoisha ili kuwaeleza yaliojiri huko bungeni na kuweza kushirikiana nao kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo badala ya kubakia huko na kujikita katika starehe mbalimbali.
No comments: