LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAGUFULI AHIMIZWA KUONDOA MAKANDOKANDO NDANI YA CHAMA.

Na:Shaban Njia;Kahama
KUFUTIA ushindi wa Dkt.John Pombe Magufuli (Pichani) alioupata katika kinyanganyiro cha kumtafuta Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga wamemkumbusha juu ya kuhakikisha anakisafisha chama hicho kwa kuwaondoa wanachama ambao sio wazalendo.

Akiongea jana na Wandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilayani Kahama Masoud Melimeli alisema kuwa Magufuli hana budi kuhakikisha kuwa anawaondoa Wananchama ambao wanaonekana kukisaliti chama.

“Unajua katika uchanguzi huu Chama cha Mapinduzi kimetumia nguvu kubwa katika kutafuta madaraka hali ambayo ni tofauti na miaka ya nyuma na hali hiyo imesababishwa na baadhi ya Viongozi waliopo katika Chama hiki ambao hawakubaliki kwa Wananchi”. Alisema Melimeli.

Pia alisema kuwa kwa sasa Chama cha Mapinduzi kimeshika tena uongozi nchini kwa awamu ya tano Mfululizo hivyo WanaCCM hawana budi kubadilika na kufanya kazi za Chama kwa ushirikiano na kuacha kuunda makundi ambayo yanawafanya kuwa na hali ya kutofautiana katika utendaji wa kazi.

Wakati huohuo ushindi wa Dtk.John Magufuli kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia (CCM) dhidi ya Mgombea mwenzake kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia chama cha Demokrasia na Maendleo (Chadema) Edward Lowassa umepokelewa furaha mjini Kahama huku vijana wengi wakipiga pushup kuashiria sasa ni kazi tuu.

Vijana hao walikuwa amejaa katika baadhi ya Mitaa katika mji wa Kahama huku wengi wao wakionekana kupiga pushup barabarani hali ambayo ilibua furaha kubwa kutoka kwa Wapenzi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliokuwa wakishangilia kwa nguvu.

“Chama cha Mapinduzi kwa sasa kimepata kiongozi Mwadilifu na mchapa kazi ambaye ataweza kukiongoza chama katika miaka mitano ijayo, na nina kuhakikishia kuwa kwa kumpata kiongozi huyo nchi itanyooka na watu watu watafanya kazi kwa bidii ili kuinua taifa hili”. Alisema mmoja wa Wanachama wa CCM Mjini Kahama Sypylau Bikampola.
Zaidi Bonyeza HAPA

No comments:

Powered by Blogger.