LIVE STREAM ADS

Header Ads

RAIS MTEULE WA TANZANIA NA MAKAMU WAKE WAKABIDHIWA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA NEC.

Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha Mwaka 2015/20 Dkt.John Pombe Magufuli (Pichani) kutoka Chama cha Mapinduzi CCM amepokea Cheti (Hati) cha Utambuzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC baada ya kuibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika jumapili iliyopita Octoba 25,2015.
Na:Binagi Media Group
Dkt.Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Mteule Samia Hassan Suluhu wamekabidhiwa cheti cha utambuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa niaba ya wajumbe wengine wa tume hiyo ambapo sherehe za kukabidhi cheti (hati) hicho imeanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Siasa na Serikali akiwemo Rais anaemaliza muda wake Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete japo mgombea wa Chadema inayoungwa mkono na Ukawa pamoja na yule wa CHAUMMA hawakuhudhuria sherehe hizo.

Shamrashamra za ushindi wa Dkt.Magufuli zinaendelea katika Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba Jijini Dar es salaam na kwa mjibu wa taratibu za NEC Rais mwenza na Makamu wa Rais mweza wanatarajia kuapishwa ndani ya siku saba baada ya kukabidhiwa cheti cha utambuzi.
Hata hivyo anatarajia kuapishwa Novemba Tano mwaka huu.
Mama Samia Hassan Suluhu ndie Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2015/20.
Zaidi Bonyeza HAPA

No comments:

Powered by Blogger.