LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YASHAURIWA KUWASOMESHA WATOTO YATIMA KATIKA SHULE BINAFSI MKOANI KIGOMA.

Na:Shaban Njia
Serikali katika Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imeshauriwa kuwasomesha watoto yatima katika shule za watu binafsi iwe ni shule za Sekondari ama msingi ambao wanaachwa na wazazi wao kwa kufariki na magonjwa mbalimbali likiwamo janga la UKIMWI kuliko kuwasomesha kupitia shule za serikali kufanya hivyo ni kuzibagua shule binafsi ambazo zote kimsingi zinatoa elimu sawa.

Ushauri huo ulitolewa juzi na mkuu wa shule ya sekondari mwalimu Tutuba iliyopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma Salehe Makunga alipokuwa akizungumza na wazazi pamoja na walezi wa watoto hao siku ya sherehe za mahafari ya kwanza ya wanafunzi wanao hitimu kidato cha nne katika shule hiyo tangu kuanza kwa masomo katika shuleni ya sekondari mwalimu Tutuba.

Aidha Makunga alimtaka mgeni rasmi Toyi Butono aliyemwakilisha mkuu wa Mkoa wa Kigoma kanali Issa Machibya amfikishie salamu  hizo kwani kuwatenga watoto yatima kutowasomesha katika shule za watu binafsi sababu ni kutotenga fedha za watoto yatima ni kuwaniyima fursa ya kupata elimu.

"Ndugu mgeni rasmi watoto hawa walianza kidato cha kwanza wakiwa 30 na hadi hivisasa wanamaliza wapo 40 pia walipokuwa kidato cha pili waliweza kuitangaza shule hii kwa kushika nafasi ya pili kwa mitihani ya iliyofanywa na shule 407 kwa kanda ya ziwa magharibi wamekuwa na mafanikio makubwa katika masomo yao licha ya kukumbana na changamoto lukuki shuleni hapa". Alisema Makunga.

Alisema kati ya wanafunzi 40 miongoni mwao 10 ni watoto yatima ambao wanatoka katika familia duni hawana wazazi ambapo shule hiyo iliweza kuchukua jukumu la kuwasomesha bure kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na kusema tangu watoto hao kumi waanze shule haijawahi kupokea sapoti kutoka serikalini hivyo alitumia fursa hiyo kuiomba serikali itenge mafugu ya kusaidia kusomesha watoto yatima wanaochukuliwa na shule binafsi.

"Ni muombe mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya asiwanyime fursa ya kielimu watoto yatima wanaohitaji kusoma katika shule za watu binafsi nashauri yatengwe mafungu ya fedha yatakayo weza kusaidia kalo za watoto wanaosoma katika shule hizo,kwani kitendo cha kutosaidiana na shule hizi ni kuzibagua shule binafsi,elimu ni ileile huo ndio ushirika". Aliongeza Makunga.

Hata hivyo mkuu huyo wa shule aliwaomba wazazi na walezi kutokata tamaa katika kuwasomesha watoto wao na ikumbukwe kuwa kila mzazi anajukumu la kuhakikisha mtoto wake anapata elimu iliyo bora zaidi hivyo aliahidi kujituma kikamilifu ilhali watoto wanaosoma katika shule hiyo atawapatia elimu bora.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne Bonevencha Richard aliwaeleza wazazi kuwa katika shule hiyo walikuwa wakisoma masomo ya sayansi kwa vitendo hali ambayo imefanya watoke na mwanga  shuleni hapo na kudai watajiendeleza endapo watafaulu vizuri kwenda kuendelea na masomo ya   kidato cha tano na sita.

No comments:

Powered by Blogger.