LIVE STREAM ADS

Header Ads

SOMA WALICHOKISEMA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA BAADA YA KINGUNGE KUCHOMOKA CCM.

Na:George Binagi
Wakazi wa Jiji la Mwanza wamempongeza kada nguri na wa siku nyingi wa Chama cha Mapinduzi CCM Kingunge Ngombale Mwiru kwa uamuzi wake wa kukihama chama hicho huku wakiunga mkono kauli yake kuwa chama hicho kimeishiwa pumzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana ikiwa ni muda mfupi baada ya Kingunge kutangaza uamuzi huo, wakazi hao ambao ni kutoka vyama mbalimbali vya siasa walisema kuwa CCM inapaswa kujitathimini upya kutokana na makada wake mhimu kukikimbia vinginevyo mwisho wake umefika na kitaondoka madarakani kwa mshangao wa ajabu.

"Hili suala la viongozi na makada wa CCM wajiondoa ndani ya chama linapaswa kutazamwa upya na si la kuuuzwa hata kidogo. Tumeshuhudia makada wakubwa kama Mawaaziri wakuu wastaafu Edward Lowasa (Mgombea Urais wa UKAWA)pamoja na Frederick Sumaye na sasa Kingunge wakijiondoa CCM. Hakika CCM inapaswa kujichunguza upya". Alisema mmoja wao bila kutaja jina.

Akitangaza jana kujiondoa ndani ya CCM mbele ya Waandishi wa Habari nyumbani kwake Kijitonyama Jijini Dar es salaam, Kingunge ambae hakutangaza kujiunga na chama chochote alisema kuwa CCM imepoteza mwelekeo huku ikiwa imelewa madaraka baada ya kutawala kwa muda mrefu lakini akatahadharisha kuwa watanzania wanataka mabadiliko na wajiamini zaidi kwani nguvu ya mabadiliko ni kubwa ikilinganishwa na nguvu ya kupinga mabadiliko hayo.

No comments:

Powered by Blogger.