LIVE STREAM ADS

Header Ads

KIFO CHA MCHUNGAJI MTIKILA CHAWAGAWA WATUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII.

Na:George Binagi
Watanzania wamegawanyika katika makundi mawili baada ya aliekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party DP Mchungaji Christopher Mtikila kufariki dunia kutokana na ajali ya gari iliyotokea jana katika eneo la Msolwa Chalinze Mkoani Pwani wakati akitokea Mkoani Morogoro katika shughuli za kisiasa.

Mgawanyiko huyo ambao zaidi ulionekana wazi wazi kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii baada ya taarifa za msiba huo, uliwahusisha wale walioonyesha masikitiko yao na wale waliokebehi kifo cha Mchungaji Mtikila ambae enzi za uhai wake katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa mwaka huu jina lake ni miongoni mwa majina yaliyondolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC katika orodha ya wagombea baada ya kutotimiza masharti ya kugombea.

Kutokana na hatua hiyo, baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walilalamikia hatua ya baadhi ya watumiaji wake kutoshtushwa na msiba huo wa Mchungaji Mtikila.

"Kwanza nianze kusema kuwa nimepokea kwa maskitiko makubwa kifo cha nguli, mchokoza fikra wa Kitaifa mzee wetu Mchungaji Christopher Mtikila. Lakini ninashangazwa na kundi la watu wanaotoa Comments za Kukejeli na kushangilia Kifo, kwa kusema eti Mungu amelipa maana alisema Ikulu sio ICU, Lowasa hapaswi kwenda Ikulu. Yaani Mtu mwenye akili unaweza kuanza kukumbuka mambo ya marehemu na kuanza kushangilia?". Ilisomeka moja ya komenti ya mtumiaji wa mitandao ya kijamii.

Hata hivyo Binagi Media Grouo inawasihi watanzania wakiwemo watumiaji wa mitandao ya kijamii kudumisha umoja wao katika nyakati kama hizi badala ya kuibua kejeli mbalimbali kwa misingi ya itikadi zao tofauti tofauti ikiwemo za kisiasa.

No comments:

Powered by Blogger.