LIVE STREAM ADS

Header Ads

TEAM ESTHER MATIKO WAWANYIMA USINGIZI WAGOMBEA WENGINE JIMBO LA TARIME MJINI.

Mgombea Ubunge (Chadema) Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko akiwahutubia Wakazi wa Jimbo hilo jana
"Jana Team Matiko tumeungana na Kamanda Daniel Marwa kutoka Musoma ndani ya Tarime Mjini kuhakikisha kuwa tunatangaza ushindi kwa kamanda wetu Esther Nicolaus Matiko kunako 0ctoba 25,2015 siku ya uchaguzi mkuu nchini.
Tulianzia mtaa wa Rembirwi Kata ya Nkende ambapo tulifanya mkutano wa kwanza na baadae mtaa wa Nkende katika Kata hiyo kwenye viwanja vya shule ya Msingi Nkende.
Katika mkutano wa pili Kamanda Matiko aliongozana na Team Matiko kutafuta kura kwa kunadi Ilani inayokwenda kuleta Maendeleo ndani ya jimbo la Tarime Mjini.
Tunawashukuru sana wananchi wa mtaa wa Nkende waliotusindikiza kwa Furaha zote zilizijaa Ndelemo na Vifijo kutoka viwanja vya Nkende shule ya Msingi mpaka Ofisi za Chadema Wilaya mtaa wa Samaltani.
Bado tunawakaribisha Makamanda Wengine (Team Matiko) kuungana nasi ndani ya Tarime Mjini. Pia napenda kuwajuza kuwa tarehe 9/10/2015 mji wa Tarime utazizima kwa ujio wa Mgombea urais Edward Ngoyai Lowasa. 
Tunawakaribisha sana wale wote mtakaoambatana na Msafara wa Mhe.Lowasa siku hiyo". Anaeleza Peter Michael Magwi kutoka Team Matiko jimbo la Tarime Mjini.
Mgombea Ubunge (Chadema) Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko akiwahutubia Wakazi wa Jimbo hilo jana
Baada ya Mkutano, Msafara ulisindikizwa hadi zilipo ofisi za Chadema Wilaya ya Tarime

No comments:

Powered by Blogger.