LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWENYEKITI WA TAASISI YA UTAWALA BORA NA UWAZI NCHINI TANZANIA KUISHTAKI SERIKALI.

Kushoto ni Mwanahabari na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kukuza Utawala Bora na Uwazi nchini Edwin Soko kiongea na wanahabari hii leo. Kulia ni Mwanahabari Gogfrey Mahonge wa Radio Maria.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Mwanahabari na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kukuza Utawala Bora na Uwazi nchini Edwin Soko anatarajia Kuishtaji Serikali ya Tanzania kwa madai ya kukiuka katiba ya nchini na kupitisha sheria ya Maudhui ya Utangazaji kwa Vyama vya siasa ya mwaka 2015 ikiwa na mapungufu kadhaa.

Soko ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza na kuongeza kuwa katika sheria hiyo ambayo iliidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, kuna baadhi ya vifungu vinavyominya Uhuru wa mtu na vyombo vya habari kupata taarifa na kusizambaza katika kipindi cha uchaguzi Mkuu.

“Ninafungua kesi ya kikatiba dhidi ya Serikali kufuatia kuwepo kwa baadhi vifungu ndani ya kanuni ndogo za maudhui ya utangazaji ya mwaka 2015, zinazokiuka katiba ya nchi na hivyo kuminya uhuru wa mtu na chombo cha habari kupata taarifa na kuzisambaza kwa mujibu wa Katiba ya nchi”. Alisema Soko.

Soko alieleza kuwa baadhi ya vifungu vya kanuni za maudhui ya utangazaji 2015, vinavyokiuka katiba ya nchi ni pamoja na kifungu cha 15(2), 6(a) na (b), 10(a), 9(2) na (3) pamoja na utangulizi wa sehemu ya tatu ya sheria hiyo unayofafanua kuwa hakuna kutangaza siku ya upigaji wa kura ambapo alibainisha kuwa kipengere hicho kina mkanganyiko ikiwa siku hiyo ni mataokeo yasitangazwe au ni vyombo vya habari kutorusha matangazo yake.

“Jambo hili lina madhara makubwa katika taifa kwani wananchi wapokonywa nguvu ya kikatiba waliyopewa katika ibara ya 18(a), (b), (c) na (d) kwa kutotakiwa kushiriki kwenye vipindi vya radio na runinga vinavyohusiana na masuala ya kisiasa kwani tunaamini kuwa hakuna sheria yoyote ya nchi iliyo juu ya katiba”. Alieleza Soko.

Tayari hatua za awali za ufunguaji wa kesi hiyo zimeisha anza ikiwa ni pamoja na kutoa tangazo la awali (notes) kwa serikali na nakala kusambazwa katika ofisi za mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nao baadhi ya wanahabari waliokuwa katika mkutano huo walielezea kuwa hatua hiyo itasaidia watunga sheria na vyombo mbalimbali vyenye mamlaka kuidhinisha sheria nchini kupitia vyema sheria na kanuni mpya kabla ya kuzipitisha na kuanza kutumika hata kama zina mapungufu kadhaa.
Wanahabari
Wanahabari
Wanahabari
Wanahabari
Wanahabari
Wanahabari
Wanahabari
Wanahabari
Mwanahabari
Mwanahabari
Wanahabari 

No comments:

Powered by Blogger.