LIVE STREAM ADS

Header Ads

ZITTO KABWE KUPITIA ACT WAZALENDO ASAKA MAJIMBO YOTE YA MKOA WA KIGOMA.

Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Zubery Kabwe
Na:Shaban Njia
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kuwa kama Wananchi wa Majimbo manane ya Uchanguzi katika Mkoa wa Kigoma watawachagua Wabunge wa Chama hicho katika uchaguzi Mkuu ujao, watahakikisha kuwa barabara ya lami kutoka katika Mji wa Nyakanazi yenye urefu wa kilometa 340 inajengwa kwa kiwango cha lami.

Kiongozi huyo ambae pia ni mgombea ubunge jimbo la Kigoma Mjini aliyasema hayo alipokuwa akimnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika Jimbo la Muhambwe Edger Mkosamali katika mkutano uliofanyika katika Kijiji Kisabwe kata ya Rugongwe jimboni humo.

Kabwe alisema Mkoa wa Kigoma kwa sasa ni moja kati ya mikoa iliyonyuma kimaendeleo hapa nchini na kuongeza Mbunge aliyepita ambaye alikuwa Mdogo wake na anayegombea kwa Tiketi ya ACT Felix Mkosamali hakuweza kuwatetea Wananchi wa Jimbo wakati akiwa Bungeni.

Aidha Kabwe alisema kuwa kama Wagombe Ubunge kwa Tiketi ya ACT watachaguliwa katika majimbo hayo manane ya Mkoa wa Kigoma, ujenzi wa barabara ya lami unaweza kukamilika ndani ya Miaka mitano ijayo na hivyo kuwaondolea adha ya usafiri wananchi wa Mkoa wa Kigoma.

“Ninawaomba Wakazi wa Kisabwe Mumchangue Edger Mkosamali kwani atawaunganisha na Masoko ya kimataifa na kuweza kuuza mazao yenu ya Mihogo pamoja na Mahindi kwa urahisi katika nchi ya Burundi na maeneo mengine hapa nchini”. Alisema Kabwe.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo Jimbo la Muhambwe Edger Mkosamali alisema kuwa kama atapata Ridhaa ya kuwaongoza Wananchi wa Jimbo la Muhambwe atahakikisha umeme unapatikana jimboni humo ikiwemo katika kata ya Busunzu kwa kuzingatia taaluma ya uhandisi aliyonayo.

“Mimi ni Mtaalamu wa Umeme nitaweza kuleta umeme katika kata ya Busunzu ikiwa ni pamoja na kuuneza katika shule za Sekondari ili kuweza kuboresha Elimu pamoja na Vitu vya Afya vilivyopo katika kata hii na mpaka hivi sasa tayari nimeishaanza kufunga umeme katika baadhi ya shule za Sekondari”. Alisema Mkosamali.

Alizitaja baadhi ya shule alizofunga umeme wa Nguvu za jua kuwa kuwa ni Mutaba Sekondari, Bitwama Sekondari, Murungu sekondari, Busagara Sekondari, Itaba Sekondari na Rubanga sekondari ambapo miradi hiyo imegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 150.

Miongoni mwa majimbo ya Mkoa wa Kigoma ni pamoja na Jimbo Kigoma Mjini, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini, Manyovu, Buyungu, Muhambwe, Kigoma Kaskazini na Kigoma Kusini.

No comments:

Powered by Blogger.