LIVE STREAM ADS

Header Ads

ZAIDI YA WATU 11 WANUSURIKA KIFO BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI WAKIWA MACHIMBONI MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Watu 11 wamenusurika kifo baaada ya kufukiwa na kifusi cha udongo katika machimbo ya Nyangarata yaliyopo katika Kata ya Lunguya katika Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Kwa mjibu wa kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Justus Kamugisha, inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tatu asubuhi baada ya watu hao kuangukiwa na kifusi cha udongo katika mashimo waliyokuwa wakichimba dhahabu huku ikidaiwa kuwa katika mashimo hayo kulikuwa na wachimbaji zaidi ya 20.

Kamugisha alifafanua kuwa baada ya tukio hilo lilifuatia tukio jingine lilitokea majira sita mchana ambapo Kamanda Kamugusha alifafanua kuwa katika tukio hilo zaidi ya watu wanne walijeruhiwa.

Kwa upande wake diwani aliyemaliza muda wake katika Kata hiyo ya Lunguya yalipo machimbo hayo Benedecto Manwari alisema kulikuwa na duara nne zilizoanguka na kujeruhi watu 11 ambao wanaendelea kupata matibabu katika kituo cha afya Lunguya.

Nae Afisa Madini Mkazi wa Wilaya ya Kahama Sophia Omary alipotakiwa kuzungumzia kuhusu tukio hilo alisema kuwa yaye hawezi kuzungumza kwani yupo safarini kuelekea eneo la tukio na kuhaidi kutoa ufafanuzi pindi atakapojiridhisha na hali ya eneo hilo.

“Jamani siwezi kutoa majibu kwa sasa, mpaka nikifika katika eneo la tukio ndipo nitaweza kutoa ufafanuzi juu ya tukio hilo na sasa naelekea huko hivyo nitawataarifu baadaye”. Alisema bi.Omari.

No comments:

Powered by Blogger.