LIVE STREAM ADS

Header Ads

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI (CCM) AAHAIDI KUMALIZA KERO ZA AFYA JIMBONI HUMO.

Na:Shaban Njia
Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika Jimbo jipya la Kahama Mjini Jumanne Kishimba amesema kuwa iwapo kama atapata ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha kuwa kero ya akina mama kujifungulia chini katika Hospitali ya Wilaya inakwisha.

Kishimba aliyasema hayo juzi wakati akiwahutubia Wakazi wa Kata ya Nyihogo Jimboni humo katika moja ya Kampeni zake zinazoendelea katika jimbo hilo huku akisisiza kuwa katika maisha huduma za afya kwa binadamu ni huhimu kuliko kitu chochote kile.

Alisema kuwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kuna jumla ya Vitanda vinane kwa ajili ya kujifungulia akinamama na kuongeza kuwa akinamama wanaojifungulia katika Hospitali ni kati ya 45 hadi 50 hali inayofanya akinamama hao kujifungulia chini.

“Dr.Magufuli (John Pombe Magufuli, mgombea urais kupitia CCM) alikuja Wilayani hapa katika Kampeni zake za kuomba kura kwa Wananchi wa Kahama kumpa ridhaa ya kuwa rais, nilimwambia kuhusu kero hiyo na yeye alikubali na kusema kuwa iwapo ataingia madarakani atahakikisha kuwa Hospiptali ya Kahama inakuwa ya Rufaa”. Alisema Kishimba.

Kuhusu ujenzi wa Zahanati katika Kata za jimbo la Kahama Mjini Kishimba alisema kuwa iwapo atapata ridhaa ya kuwaongoza Wananchi wa Kahama atahakisha kuwa maeneo ambayo ujenzi wa Zahanati ulikuwa unaendelea na haujamalizika atakodi majengo ya Watu binafsi ili huduma za afya ziweze kuondelea badala ya kusubiri zahanati kuisha.

“Haiwezekani tushindwe kukodi nyumba binafsi kwa ajili ya huduma za kiafya wakati Waganga wa kienyeji wanakodisha nyumba na kuendelea na shughuli zao ikiwa ni sambamba na kujenga nyumba za nyasi kama wodi za Wagonjwa”, Alisema Kishimba.

Nae Mgombea Kiti cha Udiwani katika Kata ya Zongomela Machibya Jidulamabambasi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama alisema;

“Tunaendelea na ujenzi Miundombinu ya Umeme kutoka katika Mgodi wa Buzwagi na muda sio mrefu kero hiyo itamalizika na kama hamuamini leo mnipe mtu ambaye nitaongozana nae hadi katika Mgodi huo kushuhudia umalizikaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya umeme ya kuja katika mji wa Kaham”. Alisema Jidulamabambasi.

No comments:

Powered by Blogger.