LIVE STREAM ADS

Header Ads

WASIMAMIZI WA VITUO VYA UCHAGUZI JIJINI MWANZA WALILIA MALIPO YAO.

Licha ya Kwamba wengi wa Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi Jijini Mwanza wamelipwa stahiki zao, bado kuna malalamiko kutoka kwa baadhi ya wasimamizi kutoka Kata za Jijini Mwanza ikiwemo Kata ya Igoma wakilalamika kutolipwa malipo yao.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Wakiwa katika Ofisi za Jiji la Mwanza wasimamizi hao wamewaeleza Wanahabari ya kwamba kuna wasimamizi wakuu ambao wanadai takribani shilingi Laki Moja na Elfu Sabini kila mmoja huku wasimamizi wasaidizi wakidai kiasi cha shilingi elfu sabini na hadi majira ya saa saba walikuwa hawajalipwa na kwamba wameelezwa kuwa malipo yao yatafanyika siku ya kesho kutwa jumatano, bila kuelezwa sababu za malipo hayo kulipwa siku hiyo.
Wasimamizi hao wamesema kuwa hawatatoka katika Ofisi ya Jiji la Mwanza hadi pale watakapolipwa stahiki zao
Wameeleza kusikitishwa baada ya kutolipwa kwa wakati stahiki zao kama mkataba wao unavyofafanua
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Tito Mahinya (Pichani) bila kutaja sababu za Wasimamizi hao kucheleweshewa malipo yao, amesema kuwa kila msimamizi atalipwa stahiki zake japo ameshindwa kufafanua ni lini malipo hayo yatafanyika kwa wale ambao bado hawajalipwa malipo yao.

No comments:

Powered by Blogger.