LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATAWANYWA KWA MABOMU YA MACHOZI JIJINI MWANZA. WENGINE WATIWA MBARONI.

Jeshi la Polisi limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya baadhi ya Wananchi waliokuwa wamefunga barabara ya Isamilo Jijini Mwanza ikiwa ni shinikizo la kutaka kuwahishwa kutangazwa kwa matokeo Rasmi ya Ubunge katika Jimbo la Nyamagana.
Na:Binagi Media Group 
Pia jeshi hilo limewatia mbaroni baadhi ya waliohusika na tukio hilo. Hali ya usalama imeimarishwa maeneo yote yanayozunguka ofisi za Jiji la Mwanza ambapo matokeo yatatangazwa kutoka ofisi hizo.
Jijini Mwanza
Jijini Mwanza
Ulinzi umeimarishwa zilipo Ofisi za Jiji la Mwanza
Wengine walikimbilia milimani
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Tito Mahinya (Pichani) amesema kuwa Matokeo hayo yatatangazwa punde tu uhesabuji wake utakapomalizika japo awali alieleza kuwa matokeo hayo yangetangazwa majira ya saa nane.

No comments:

Powered by Blogger.