LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATENDAJI HALMASHAURI YA MSALALA WALALAMIKIA OFISI YA MKURUGENZI KATIKA KUTOA AJIRA.

Na:Shaban Njia
Makaimu Watendaji wa Vijiji 46 katika Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wametoa malalamiko yao kwa kuilaumu Ofisi ya Mkugenzi wa halmashauri hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa hawakupewa kipaumbele katika kuidhishwa kuwa Watendaji kamili na badala yake wamenyimwa ajira na kuajiriwa watu kutoka mikoa mingine.

Juzi Watendaji hao walisema kuwa wamekuwa wakikaimu nafasi hiyo kwa muda wa zaidi ya miaka minane huku wakiahidiwa kuidhinishwa kuwa Watendaji kamili pindi ajira zitakapotoka hali ambayo imekuwa tofauti na matarajio yao.

Mmoja wa watendaji hao Eliasi Kazimoto alisema kuwa Halmshauri ya Msalala ilitoa tangazo la Kazi za utendaji na kuwaomba watume vyeti vyao vya sekondari hali ambayo kati ya Watendaji 46 waliotuma vyeti ni watatu tu walioitwa katika usaili na hata hivyo hawakuweza kupata kazi.

Kazimoto ambaye alikuwa ni Kaimu Mtendajio wa Kijiji cha Nyamididi aliendelea kusema kuwa kwa sasa katika halmashauri ya Msalala hakuna Kaimu Mtendaji wa Kijiji hata mmoja na kuongeza kuwa wote wameishatolewa na kuwekwa watu wengine kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

“Hatujalipwa posho kwa miezi 12 pia za utendaji wetu, na kila mwaka tuliahidiwa na kupitishwa katika baraza la Madiwani kuwa kila Mtendaji alipwe kiasi cha shilingi 60,000 kwa Mwezi lakini mpaka kufikia hivi sasa hakuna aliyelipwa fedha hizo”. Alisema Kazimoto.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa alipotakiwa kuzungumzia malalamiko hayo alisema kuwa habari hizo si za kweli na kwamba mwenye malalamiko afikishe malalamiko hayo katika ofisi yake.

No comments:

Powered by Blogger.