LIVE STREAM ADS

Header Ads

AUDIO: WAKILI WA CHADEMA, WANANCHI NA MBOWE WAZUNGUMZIA MWILI WA MAWAZO KUAGWA JIJINI MWANZA.

Mvutano baina ya Polisi na Chadema juu ya shughuli za kuuaga mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoani Geita marehemu Alphonce Mawazo (Pichani) zilizokuwa zimepangwa kufanyika Jijini Mwanza umetinga Mahaka Kuu Kanda ya Mwanza baada ya polisi kuzuia mwili huo kuagwa Jijini Mwanza kutokana na hofu ya Kiusalama pamoja mlipuko wa Kipindupindu Mkoani Mwanza.

Mwafaka wa mvutano huo unatarajiwa kuanza kutolewa leo Novemba 24,2015 ambapo Mahakama hiyo itaanza kusikiliza shauri lililowasilishwa jana Novemba 23,2015 na Chadema Mahakamani hapo. Mawazo aliuawa Novemba 14 na watu wasiojulikana Mkoani Geita.
Bonyeza Play Hapo Chini Kusikiliza Hatua zilizochukuliwa  Bonyeza HAPA Kutazama Picha za Mahakamani

No comments:

Powered by Blogger.