LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAHAMA WAIPONGEZA SERIKALI KUWARUDISHA SHULENI WANAFUNZI WALIOJIFUNGULIA MAJUMBANI.

Na:Shaban Njia
Wakazi pamoja na Wadau wa Elimu katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga wamepongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwarudisha wanafunzi wa kike Madarasani kuendelea na Masomo yao pindi wanapopata ujauzito na kujifungua  wakiwa Mashuleni.

Wakazi hao jana walisema kuwa kitendo cha serikali kuona umuhimu wa kuwarudisha Wanafunzi hao waliopata ujauzito na kujifungua wakiwa mashuleni kutasadia katika kuwaepusha  utumikishwaji wa kazi nyingi huku hasa ajira za baa wakiwa bado ni wadogo.

Pia walisema kuwa ni vizuri kwa Serikali kama imeweza kuliona suala hilo kwani lilikuwa likimweka mototo wa kike katika maingira ya kuona kuwa wananyanyaswa kijinsia kwani wanapopa ujauzito wakiwa mashuleni anayefukuzwa ni mtoto wa kike ni sii wa kiume.

Aidha waliendelea kusema kuwa unapomfukuza mtoto wa kike shule wakati akiwa mjamzito pia kunapoteza nguvu kazi ya taifa kwa siku ya baadaye kwani hata uchumi wa nchi unaweza kushuka kutokana na kutokuwa na kundi kubwa la wasomi hususani kwa Wanawake.

Mmoja wa  Wananchi hao ambaye pia ni Mratibu wa Afya ya uzazi na Balehe  kwa Vijana kutoka katika shirika lisilo la Kiserikali la KIWOHEDE Faraja Shabani alisema kuwa wanashukuru kwa Serikali kuliona kwa umakini suala hilo na kuongeza kuwa kama mtoto huyo wa kike akirudishwa shuleni hakuna atakayeweza kurudia kosa hilio.

“Tunaiomba Serikali iweke utaratibu mzuri kwa Mwanafunzi aliyepata ujauzito kwani kipindi akifungua na kumaliza kulea mtoto apate kurudi shuleni nakundelea na pale alipoishia kwa kipindi hicho”, Alisema Faraja Shabani Mratibu wa Kiwohede Wilaya ya Kahama.

Aidha Shabani aliendelea kusema kuwa ukosefu wa Elimu kwa mtoto wa kike pia kunaweza kukawa ni moja ya sababu ya kundi hilo kujingiza katika biashara mbalimbali haramu kama vile za kuuza miili yao hali ambayo inatokana na kukosa ajira kwani kwa wakati huo wanakuwa hawana sehemu yeyote ya kuwazalishia kipato.

“Unajua ndugu mwandishi wa Habari hata watoto wetu wanaojiingiza katika biashara haramu ya kuuza miili yao pina inaweza ikawani moja ya sababu za kukosa Elimu kwa wakati muafaka au walipata ujauzito wakiwa mashuleni ni kuzuiliwa kuendelea na masomo hali ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuendeslea kushamiri kwa kundi hilo siku hadi siku”, Alisema Shabani.

No comments:

Powered by Blogger.