NAIBU KAMISHNA MKUU UNHCR NA UJUMBE WAKE WATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Uongozi wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi ukiwa katika kikao na Ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) uliotembelea Wizara hiyo. Wa pili kulia ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia) akizungumza na ujumbe wa Shrika la Umoja wa
Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) (haupo pichani) uliotembelea Wizara hiyo
ambapo masuala mbalimbali kuhusiana na wakimbizi yalijadiliwa. Tanzania
ni mojawapo ya nchi zinazohifadhi wakimbizi, hususani kutoka Ukanda wa Maziwa
Makuu.
Kulia ni Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bi. Kelly Clements
akizungumza katika kikao na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (haupo
pichani) wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi. Katikati ni Mkurugenzi wa UNHCR, Kanda ya Afrika na kushoto ni Mtendaji
Msaidizi wa Naibu Kamishna Mkuu wa UNHCR, Bi. Geraldine Salducci.
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi
katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (Kushoto) akizungumza katika
kikao cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na ujumbe wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wakati ujumbe huo ulipotembelea Wizara.
Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
(Picha zote na Abubakari
Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments: