LIVE STREAM ADS

Header Ads

WACHIMBAJI WADOGO WADOGO WA DHAHABU MKOANI SHINYANGA WATEGEMEA NEEMA KUTOKA KWA RAIS MAGUFULI.

Na:Shaban Njia
Baada ya Dkt.John Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, huenda ikawa neema kwa kundi la Wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu kutokana na maeneo yao mengi wanayovumbua kwa ajili ya kuendesha shughuli za uchimbaji kuchukuliwa na wawekezaji wakubwa wenye leseni za uchimbaji huku wakishindwa kuyaendeleza maeneo hayo.

Wakiongea juzi muda mfupi baada ya Dkt.Magufuli kuapishwa kuwa Rais, Wachimbaji wadogowadogo kutoka Mkoani Shinyanga walisema kuwa wamefarikijika baada ya kusikia kiongozi huyo amepewa ridhaa ya kuongoza taifa la Tanzania kwa kuwa atakuwa msaada mkubwa kwa hilo nchini.

“Sisi kama Wachimbaji wadogowadogo wa Madini ya dhahabu katika Mkoa wa Shinyanga ni moja kati makundi makubwa yaliompa kura nyingi Dkt.Magufuli na  kutokana na utendaji wake wa kazi na kuwa kiongozi Mwadilifu katika Serikali tunategemea mabadiliko makubwa hasa kwa wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakivumbua maeneo ya uchimbaji na badala yake kunyang’anywa na wawekezaji wakubwa. Alisema Nicodemus Majabe ambae ni Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu Mkoani Shinyanga.

Aidha alibainisha kuwa kuna baadhi ya maeneo Mkoani Shinyanga kama vile ya Kalole, Mwanziro pamoja na Nyangalata wamekuwa wakiombwa kupewa umiliki wake kwa ajili ya shughuli zao za uchimbaji lakini hali imekuwa ni tofauti huku akisema kuwa wana matumaini na kauli ya Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu kwani itaweza kuwasaidia kupata maeneo ya uchimbaji wa dhahabu.

No comments:

Powered by Blogger.