LIVE STREAM ADS

Header Ads

APEC KUTOA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI,POLISI JAMII NA UJASIRIMALI KWA MADREVA BODABODA KAHAMA

Na:Shaban Njia
UMOJA wa madreva pikipiki maruufu kama (BODABODA ) Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, wametakiwa kushirikiana  na kutoa taarifa kwanye vyombo vya usalama pindi watakapomshuku mtu kuwa mbaya kwa jamii ili kuepusha vitendo viovu vinavyoendelea vya madreva pikipiki vya kuuwawa na watu wasiofahamika wakiwa na lengo la kuwapora pikipiki zao.

Kauli hiyo ilitolewa juzi iliyopita na Mkurugenzi Msaidi wa Shirika la APEC Faustin Martin katika kilele ya kuhitimisha mafunzo ya utoaji wa elimu ya usalama barabarani,Polisi jamii pamoja na ujasiliamali wilayani hapa ikiwa ni njia mojawapo ya kupuguza ajali zisizolazima.

Alisema kuwa shirika la APEC limekuwa likitoa mafuzo hayo kwa madreva pikipiki na makundi mbalimbali hapa nchi ambapo mafunzo hayo yametolewa katika mkoa wa Mwanza,Simiyu,Mara,Shinyanga,Tanga pamoja na Mkoa wa Dar-es-salaam sambamba na kuwapatia elimu ya ujasilimali vijana wanaoshinda vijiweni bila kujishughulisha ili kujikimu katika maisha.

“Tunatoa elimu ya usalama baraabarani kwa madreva pikipiki,pia elimu ya Polisi jamii na elimu ya ujasilimali ili kupunguza vijana wanakuwa na dhana ya kutegemea na kusibili ajira toka serikalini na katika mafunzo hayo tunawapatia mbinu ya kumtambua nani mzuri na nani mbaya ili iwe rahisi kwao kutoa taarifa katika vyombo vya uslaama”. Alisema Martin.

Aidha alisema kuwa kwamafunzo ambayo wamewapati madreva hawa wanategemea watatii sheria bila shuruti,nakuongeza kuwa anategemea madreva watashirikiana vema na jeshi la polisi kutoa taarifa ili kuwafichua wahalifu bila kuvunja amani iliyopo, ambapo mafunzo hayo yalijumuisha wananchama 89 huku wakiume wakiwa 85 na wakike wakiwa wanne.

Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa aliwataka madreva pikipiki kuitumia vema elimu waliyoipata toka katika Shirika la APEC kwa kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu kutokana na wilaya ya Kahama kuingiliwa na watu kutoka nje na ndani ya Kahama wakijifanya ni wafanyabiashara huku ni wahalifu.

“Ndugu zangu madreva mliopata elimu hii,nadhani ajari barabarani zitapungua kwa kiasi kikubwa na kama mwanzoni ajali zilikuwa 20 kwa mjibu wa usalama barabarani  kwa siku sasa kutakuwa na jaili 5,Lakin kumbukeni pia kuitumia vema elimu ya polis jamii kwakutoa taarifa kwajeshi la polis na mnavyojua Kahama yetu inamwingiliano wawatu kutoka Rwanda,Burundi,Uganda wanaingia nchi kwakishingizio cha kufanya biashara”. Alisema Kawawa.

Nae katibu wa umoja wa waendesha pikipiki(BODABODA) Hossea Soni alisema kuwa wataitumia vema elimu waliyoipata toka katika shirika la APEC ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama pindi litakapojitokeza tatizo na kuongeza kuwa wataendelea kuwahamasisha na wengi pindi mafunzo yatakapoanza kwa mara nyingine wajitokeze kwa wingi.

Hata hivyo Hosea aliwataka wendesha pikipiki wenzake kutii sheria bila shuru pindi anapokesa kwakupita barabara ambayo hakupaswa kupita ili kuonesha mfano kwa madreva wengine kwa yale aliyojifunza ili na wengine ambao hawakupata mafunzo ya usalama barabarani,elimu ya ujasilimali pamoja na polisi jamii wajifunze toka kwako.

“Ndugu zangu naombeni sana tuitumie elimu tuliyoipata kwa umakini zaidi ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za barabarani na pindi inapotokea tatizo na polisi wa usalama barabarani anapokusimamisha,simama na msikilize ili kuonesha mfano kwa wenzako”. Alisema Soni.

No comments:

Powered by Blogger.