LIVE STREAM ADS

Header Ads

FOUNDATION KARIBU TANZANIA YAIASA JAMII KUTOKOMEZA UKATILI MAJUMBANI.

Judith Ferdinand, Mwanza
JAMII imeombwa kushirikiana na Serikali pamoja na Taasisi mbalimbali, kupinga na kufichua wale wote wanaowafanyia vitendo  vya kikatili watoto majumbani, ili kukomesha na kutokomeza  changamoto hiyo nchini.

Kutokana na utafiti uliofanya na shirika lisilo la kiserikali linalo hudumia watoto wanaofanyiwa vitendo vya kikatili majumbani la Foundation  Karibu Tanzania (FKT),lililopo mkoani hapa na kubaini sababu ya jamii kutokuwa tayari kufichua  vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ni kuogopa kuvunja mahusiano yao pamoja na usalama wa maisha yao.

Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa shirika la FKT Benard Makachia wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili dhidi ya watoto majumbani.

Makachia alisema kutokana na jamii kutokuwa na elimu juu ya madhara na umuhimu wa kufichua watu wanaowafanyia vitendo hivyo watoto, kupitia shirika hilo wameanza kuelimisha jamii  ambayo kwa kiwango kikubwa sasa wameweza kujitokeza kutoa taarifa.

Naye Kamanda wa Polisi wilaya ya Ilemela (OCD), Tryphone Kisha alisema jamii ijikite kuzuia ukatili usitokee kwani unapotokea unaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi kama usalama wa aliyetoa taarifa.

Kisha aliliomba shirika la FKT kutoa  huduma kwa watoto wanaishi katika mazingira magumu(watoto wa mtaani), kwani na wao wanafanyiwa vitendo vya kikatili ili kupunguza na kutokomeza ongezeko la watoto hao.

Pia alisema, jeshi la polisi litashirikiana na jamii pamoja na FKT kuhakikisha wanatokomeza suala zima la ukatili dhidi ya watoto majumbani.

Kwa upande wake Meneja mradi wa  FKT Melchizedek Massola  alisema, shirika hilo limejikita kuelimisha jamaa na kuhimiza juu ya kuacha kuwafanyia ukatili watoto, kwani tunawasababishia matatizo makubwa ikiwemo ulemavu.

No comments:

Powered by Blogger.