LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAYA 65 KATA YA ISAKA KAHAMA HAZINA VYOO, HATARINI KUKUMBWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU.

Na:Shaban Njia
WAKAZI wa vijiji vya kata ya Isaka katika halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama, Shinyanga wako mbio kukumbwa na magojwa yamlipu ukiwemo ugonjwa kipindupindu huku zaidi ya kaya 65 katika katahiyo, hazina vyoo hali ambayo wananchi kujisaidi vichakani.

Hayo yalibainishwa jana na Afisa Mtendaji wa kata ya Isaka Nicholausi Maya katika uzinduzi wa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya usafi ifikapo Disemba 9 mwaka huu, ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,john Magufu kufanya usafi ifikapo siku hiyo.

Maya alisema kuwa licha ya Rais kuagiza ifikapo disemba 9 mwaka huu kila mtanzania kufanya usafi ipo haja ya serikali kuzifunga baadhi ya nyumba ambazo hazina vyoo ambapo zaidi ya kaya 65katika kata ya isaka zimebainika kutokuwa na vyoo hali ambayo inaweza kupelekea kulipuka kwa magonjwa ya mlipuko.

Alisema kuwa kufanya usafi ni jukumu la kila Mtanzania aliyopo katika eneo husika,hata kama sio mkazi wa maeneo hayo anatakiwa kushirikiana na wenzake kutekeleza agizo la Rais kufanya usafi ifikapo disemba 9,nakuongeza kuwa atakaekwenda kinyume na agizo hilo hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.


“Kila mtanzania anatakiwa kufanya usafi ifikiapo siku ya Disemba 9 ambayo ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya Uhuru kitaifa lakini kutokana na agizo la Rais wetu kuwa siku hiyo inatakiwa kuwa siku ya watanzania wote kufanya usafi katika maeneo yanayotuzunguka haina buku kutekeleza agizo hilo ili kuenzi kauli mbio ya HAPA KAZI TU” Alisema Afisa Mtendaji Maya.


 Katika hatua nyingine Maya alisema kuwa kwa kushirikiana na timu ya maafisa wa kata pamoja na maafisa wa jeshi la polisi watahakikisha kila mkazi wa kata ya mwakata anafanya usafi katika maeneo yake, nakuongeza kuwa atakaebainika katika eneo lake hakufanya usafi atatozwa faini ya shilling, Millioni.1 au kwenda jela miezi mitatu.

Nae Bwana Afya wa kata hiyo Elias Nchunga alisema kuwa kila mtanzania anatakiwa kufanya usafi kwa nafasi yake kwakuzingatia sheria na kanuni za afya na kuongeza kuwa kwa mamantile atakaebainika mazingira yake ya kibiashara ni machafu atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja
na kufungiwa biashara.


“Kabla viongozi wangu wa ngazi za juu hawajanichukulia hatua ni lazima mimi nikuchukulie hatua ili kuepukana na maafa makubwa ambayo yanaweza kutokea pindi mazingira yanapokuwa sio rafiki kwa mwananchi,hasa kwa mamantilie atakaekutwa katika biashara yake kunauchafu na hakufanya usafi,maafisa tutachukua hatua ya kufunga biashara yake",alisema Nchunga.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Zabroni Donge alisema kuwa amewataka wakazi wa kaya hiyo kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kuhifadhi taka ngumu  hali ambayo itapunguza utupwaji wa takataka ovyo ili kufanya mazingira kuwa safi na salama.

“Tengeni maeneo ya kuhifadhia takataka maaana katika maeneo hayo sijaona wapi mnatunzia  takataka, kumbukeni kwamba pindi mtu anapokuwa naumwa ugonjwa wa kipindupindu anakuwa amekuwa kinyeshi kibicho hivyo basi fanyani usafi ili kuepukana na magonjwa ya mlipuka ambayo yatakuingiza gharama zisizo na msingi”,alisema Donge.

No comments:

Powered by Blogger.