LIVE STREAM ADS

Header Ads

KISHIMBA ATOA VIFAA VYA SHILINGI MILIONI 27 KATIKA WODI YA WAZAZI ILI KUBORESHA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO.

Na:Shaban Njia
KATIKA kuhakikisha ahadi walizotoa wakati wa Kampeni za kuomba Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini Mkoani Shinyanga zinatekelezeka , Mbunge wa jimbo hilo Jumanne Kishimba ametoa Msaada wa Vifaa mbalimbali katika wodi ya Wazazi katika Hopitali ya Wilaya kwa lengo na kukuza huduma za mama na Mtoto.

Akikabidhi Vifaa hivyo kwa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Bruno Minja, Kishimba alisema kuwa ameamua kutoa Vifaa hivyo katika wodi hiyo ya wazazi kwa lengo kukuza huduma za watoto na akinamama wanakwenda kujifungua katika Hospitali hiyo.

Alisema kuwa hali ya Hospitali ya Wilaya ya Kahama ni mbaya na malalamiko ni mengi kuhusu huduma zinazotolewa hasa katika wodi ya wazazi na Akinamama wajawazito hali ambayo ilinifanya niguswe na hali hiyo na kutoa msaada huo.

Alivitaja baadhi ya Vifaa alivyotoa katika Hospitali hiyo kuwa ni pamoja na Mashine ya Oxgeni, Mashine ya kufyonza vimiminiko vinavyotka kwa mama Mjamzito baada ya kujifungua, Taa za kumulika wakati wa kujifungua,  Vitanda vya kujifungulia akinamama vikiwa 11 , Vifaa vya kusafishia pua kwa watoto,  Masine ya kupima mapigo ya moyo kwa mtoto akiwa tumboni, glovs, buti pamoja na mipira ya mkojo.

Aidha Mbunge huyo wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba alisema kuwa vifaa hivyo jumla vyote vina thamani ya shilingi milioni 27 huku akihaidi kuendelea kusaidia Hospitali hiyo katika masuala ya ukarabati ambayo tayari umeshaanza kufanyika katika baadhi ya wodi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa  Hospitali ya Wilaya ya Kahama Dr, Bruno Minja alisema kuwa anashukuru kwa msaada huo ambao ulikuwa ni muhimu kwao kwani  Hospitali yake ina changamoto kuwa kwani kwa siku jumla ya akinamama wanaojifungua ni kuanzia 20 hadi 25 huku  vitanda alivyokuwap[o awali vikiwa nane tuu.

Aidha Mganga Mkuu hiyo aliendelea kusema kuwa ili kupunguza idadi ya akinamama wajawazito  kuja kujifua kwa idadi kubwa kutoka Vijijini aliwaomba Madiwani wa Halmashauri ya Mji huo kuhakikisha kuwa wanawahimiza Wananchi katika kata wanazotoka kuweza kujiandikisha katika mfuko wa Bima ya Afya ili kupunguza wimbi la Wagonjwa.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba alisema kuwa Halmashauri yake haina Ruzuku kutoka Serikali kwa sasa  na kuongeza kuwa kwa sasa wanatumia fedha kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri hali ambayo matumizi yake yanakuwa ni makubwa kuliko fedha  zinazotolewa kwa huduma za afya katika Hospitali hiyo.

Alisema kuwa fedha za Halmashauri hiyo zina matumizi mengi mbali na yale ya kiafya na kuongeza kuwa kwa sasa kuna kazi kama za ujenzi wa Mabarabara katika Halmashauri pamoja na Madaraja katika maeneo ya kata 20 yanazunguka Mji huo.

No comments:

Powered by Blogger.