LIVE STREAM ADS

Header Ads

KISHIMBA: VIJANA TUMIENI VIONGOZI WA DINI KUPATA USHAURI JUU YA MAAMBUKIZA YA UKIMWI.

Na:Shaban Njia
VIJANA Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kuwasikiliza Watu mbalimbali wanaowazidi umri ikiwa ni pamoja na Viongozi wa Dini ili kupata ushauri mzuri kuhusu masuala mazima yanayohusu Ugonjwa wa UKIMWI na dalili zake.

Wito huo ulitolewa wiki hii na Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba wakati akiongea na wakazi wa Mji wa Kahama  katika tamasha la Vijana  lililoambatana na upimaji wa Virusi vya Ukimwi.

Kishimba ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika tamasha hilo ambao lilidhaminiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la GUTZ FOUNDATION la Jijini Dar Es Salaamu alisema kuwa kwa Vijana vijana wengi wamekuwa wakiambukizwa Virusi vya Ukimwi kutokana na kutopata mawaidha kutoka kwa watu wanaowazidi Umri.

“Tumieni watu wanaowazidi umri pamoja na Viongozi wa Dini katika kupata Elimu juu ya Ugonjwa wa Ukimwi hali ambayo itawasaidi katika kubadili tabia na kutenda matendo yalio mema ikiwa ni pamoja kutumia kinga wakati wa kujamiiana”, Alisema Kishimba Mbunge wa Jimbo la Kahama.

Pia Kishimba aliwataka Vijana kuacha ngono zembe na kutumia kinga wakati wa kufanya tendo la ndoa kwani hali ya maambukizi ua Ugonjwa huo hasa katika Wilaya ya Kahama yapo  katika kiwango cha hali ya juu kutokana na mji huo kuwa na mwingiliano mkubwa wa watu kutoka katika sehemu mbalimbali za hapa nchini na nje ya nchi.

“Mji wa Kahama unakuwa kwa kiwango cha juu na huwiz kupata takwimu sahihi kuhusu maambukizo ya Ugonjwa huo kwani kuna watu wanaingia na kutoka kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi kuja kufanya biashara mbalimbali hali ambayo huwezi kupata tawimu zilizo sahihi”, Aliongeza Kishimba.

Kwa upande Dr.Damiani Chagi kutoka shirika lisilo la Kiserikali la Gutz Foundation alisema kuwa katika tamasha hilo pia kumekuwepo na zoezi kubwa la upimaji wa damu ili kuhamasisha wananchi kujua afya zao hali ambayo itachangia kuondokana na woga ulipo kwa baadhi ya watu kuogopa kupima afya zao.

“Tunaendesha zoezi la upimaji wa Damu kwa hiyari kwa mtua ambaye anataka kufanya hivyo , lengo na kuhamasisha  watu kujua afya zao na mpaka kufikia muda wa saa tisa mchana huu tayari jumla ya watu 574 wamekwishajitokeza kupima na pia hadi kufikia muda wa saa 12 jioni tutakapofunga zoezi hili tutakuwa tayari tumepata takwimu halisi”, Alisema Dr, Damian Chogi.

No comments:

Powered by Blogger.