LIVE STREAM ADS

Header Ads

KITUO CHA WAKIMBIZI NDUTA KILICHOPO MKOANI KIGOMA CHAHIFADHI WAKIMBIZI WENGI.

Na:Shaban Njia
SERIKALI katika Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imesema kituo cha Wakimbizi cha NDUTA kilichopo wilayani humo kinahifadhi zaidi ya Wakimbizi takribani 60,000 raia wa nchi jirani za Burundi, Rwanda pamoja na Congo.

Aliyasema hayo Mkuu wa Wilaya hiyo Lucy Msafiri wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii, ambapo alisema kituo hicho kinapokea zaidi ya wahamiaji hao haramu,raia wa nchi jirani za Burundi,Rwanda na Congo.

Msafiri alisema kituo cha nduta kinapokea Wakimbizi karibia 60,000 na idadi kubwa ya wakimbizi hao ambayo ni sawa na asilimia 50 ni raia wa nchi ya Burundi na kuongeza kuwa ongezeko hilo linatokana na mapigano yanayoendelea nchini humo.

“Tunamshukuru Mungu kambi yetu ya wakimbizi ni kubwa hali ambayo inaifanya kuhimili kishindo cha wakimbizi kwa kubeba idadi kubwa ya watu hao ambapo mwanzo walikuwa elfu 35 na hadi kufikia sasa tunaidadi ya wakimbizi elfu 60 na wote wapo chini ya uangalizi wa serikali,”alisema Msafiri.

Alisema kuwa serikali inaendelea kuwapatia huduma mbalimbali za kibinadamu kama chakula,mavazi,Afya sambamba na huduma muhimu za kijamii kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya serikali huku wakiwa chini ya uangalizi wa serikali.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Mhambwe kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Atashasta Nditiye alisema kuwa suala la wakimbizi kutoka nchi jirani za Burundi, Rwanda na Congo atalisimamia kwa kusaidiana na serikali ili kuhakikisha kuwa wanaingia kwa kufuata sheria na taratibu za nchi.

No comments:

Powered by Blogger.