LIVE STREAM ADS

Header Ads

MADIWANI MANISPAA YA ILEMELEMA WALA KIAPO CHA KUWATUMIKIA WANANCHI KWA UADILIFU.

Judith Ferdinand, Mwanza
Jumla ya Madiwani 27 katika Jimboni Ilemela Mkoani Mwanza, wamekula kiapo cha kuwatumikia wananchi katika kipindi cha miaka mitano ijayo ya awamu ya kwanza ya serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Wakiapa leo mbele ya Hakimu Mkazi  wilaya ya Ilemela Stellah Kiama, katika uwanja wa halmashauri ya wilaya hiyo, Madiwani hao walisema kuwa wapo tayari  kuwatumikia wananchi.

Kati ya Madiwani hao, 19 walichaguliwa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, huku saba wakiwa ni wale wa viti maalumu pamoja na Mbunge wa  jimbo hilo Angelina Mabula.

Mkuu wa Wilaya hiyo Manju Msabya aliwataka Madiwani hao, kuwatumikia wananchi kulingana na mahitaji yao, bila ya kujali itikadi ya vyama walivyotoka.

Pia aliwaomba Madiwani hao, kushirikiana na kushauriana katika kutenda kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya jimbo, bila ya kujali itikadi ya vyama.

Hata hivyo aliwaomba, watendaji Wa Kata kutoa ushirikiano kwa Madiwani, pale wanapoitaji taarifa za Kata zao.

Nae Mbunge wa jimbo hilo Angelina Mabula, aliwaomba Madiwani hao kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni, ili kutatua na kuzikabili changamoto zinazoikumba jamii.

No comments:

Powered by Blogger.