LIVE STREAM ADS

Header Ads

YOUNG WOMEN'S CHRISTIAN ASSOCIATION (YWCA) TAWI LA MWANZA WAADHIMISHA KILELE CHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.

Na:George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group (BMG)
Chama cha YWCA (Young Women's Christian Association) Tawi la Mwanza, jana (Desemba 10,2015) kimeshiriki maadhimisho ya kilele cha Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia duniani ambapo kiliiasa jamii kushirikiana na serikali ili kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokomezwa. 

Maadhimisho hayo yalifanyika katika Uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali pamoja na dini.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Debora Osarya ambae ni Katibu wa YWCA Tawi la Mwanza aliwaomba wanajamii kushirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali ili kufichua na hatimae kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii.

Chama cha YWCA Tanzania kilianzishwa mwaka 1959 nchini ambapo hadi sasa kina matawi 22 yenye wanachama wapatao 4,000 kote nchini ambapo makao makuu yake yako Jijini Dar es salaam. Miongoni mwa malengo ya YWCA ni pamoja na kujenga uongozi na sauti sawa kwa wanawake katika jamii na kuhamasisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Baraka Nyamsinda ambae ni Afisa Tawala Manispaa ya Ilemela akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela ambae alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo. Alisema Manisaa ya Ilemela iko tayari kushirikiana na YWCA kwa ajili ya kuhakikisha kuwa ukatili wa kijinsia unatokomezwa katika jamii.
Mratibu wa Kampeni ya Tamar nchini, Jesca Ndana akizungumza katika Maadhimisho hayo. Alisisitiza wananchi kufichua vitendo vya ukatili katika jamii ili kuwa na jamii salama. Kampeni ya Tamar inawahamasisha wanajamii kupaza sauti ili kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia na hatimae kuvitokomeza kabisa.
Kushoto ni Katibu wa YWCA Tawi la Mwanza, Debora Osarya akisoma risala katika kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani yaliyofanyika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. Aliomba wanajamii kushirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali ili kufichua na hatimae kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii.
Wanafunzi wa Shule ya msingi Sabasaba wakisoma shairi katika kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani yaliyofanyika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza
Wanafunzi wa Shule ya msingi Sabasaba wakionyesha igizo linalozuia ukatili wa kijinsia katika kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani yaliyofanyika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza
Wanafunzi wa Shule ya msingi Sabasaba wakionyesha igizo linalozuia ukatili wa kijinsia katika kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani yaliyofanyika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza
Mmoja wa wageni waalikwa akichangia Mdahalo, ambapo Mada iliangazia juu ya Ukatili kwa Wanawake
Mshereheshaji
Godfrey Salum kutoka YWCA Mwanza akichangia Mdahalo
Mratibu dawati la Jinsia kitengo cha polisi Manispaa ya Ilemela akichangia Mdahalo
Kulia ni Ustadhi Yasin Mrisho akichangia Mdahalo
Mwanahabari Simba Uranga akichangia Mdahalo
Mmoja wa wanafunzi akitoa maoni yake
Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia
Maandamano ya wanafunzi wa shule ya msingi Sabasaba, Manispaa ya Ilemela wakiwa katika maandamano ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia
Burudani kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi Sabasaba
Wanafunzi wa shule ya msingi Sabasaba wakifurahia igizo
Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia
Kauli Mbiu ya YWCA ni Amani Nyumbani, Amani Duniani, Elimu Sawa Kwa Wote.
Bonyeza HAPA Kusoma Kuhusu Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani.

No comments:

Powered by Blogger.