LIVE STREAM ADS

Header Ads

NGAMIA WANOGESHA SIKUKUU YA CHRISTMAS KATIKA MJI WA TARIME MKOANI MARA.

Mmoja wa Wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime akiwa amepanda juu ya Mnyama NGAMIA ikiwa ni katika kusherekea Sikukuu ya Christmas iliyoadhimishwa jana Desemba 25,2015 kote duniani.
Na:Binagi Media Group
Shughuli nzima ilisimamiwa na Kituo cha Utalii wa Kiutamaduni (Serengeti Cultural Centre) kutoka Wilayani Serengeti Mara ambacho katika kuhamasisha suala la Utalii wa ndani, kilitoa fursa kwa wananchi kufika katika Uwanja wa Sabasaba mjini Tarime na kupiga picha na mnyama ngamia na kufurahia michezo mbalimbali na mnyama (Wanyama) huo.

Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo hicho Joshua Nyansiri aliiambia BMG kuwa hatua hiyo inasaidia kukuza utalii hususani ule wa asili huku mamia ya wakazi wa Mji wa Tarime waliofika kushuhudia michezo mbalimbali na mnyama (wanyama) huyo wakifurahia zaidi hususani wakati wa kumpanda juu na kupiga nae picha.
Usikose leo katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Tarime ili kupiga picha na mnyama ngamia.
Mmoja wa Wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime akiwa amepanda juu ya Mnyama NGAMIA ikiwa ni katika kusherekea Sikukuu ya Christmas iliyoadhimishwa jana Desemba 25,2015 kote duniani.
Mmoja wa Wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime akiwa amepanda juu ya Mnyama NGAMIA ikiwa ni katika kusherekea Sikukuu ya Christmas iliyoadhimishwa jana Desemba 25,2015 kote duniani.
Hii inasaidia kukuza utalii wa ndani
Watoto wakipiga picha na mnyama ngamia
Wengi walifurahia kupiga picha na mnyama ngamia
Baadhi waliduwaaaa
Wengine walipigwa na butwaa
Wapo ambao walikuwa hawaamini kila wakiona mnyama ngamia anavyowabeba wanadamu
Wengine walichukua kumbukumbu
Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha Serengeti Cultural Centre, Joshua Nyansiri (mwenye kofia) akiuza tiketi kwa waliokuwa wakihitaji kupiga picha na mnyama ngamia.
Usikose leo katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Tarime ili kupiga picha na mnyama ngamia.
Bonyeza HAPA Kutazama Picha Zaidi

No comments:

Powered by Blogger.