LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERENGETI CULTURAL CENTRE WAWAKOSHA WAKAZI WA MJI WA TARIME MKOANI MARA.

Katika msimu huu wa Sikukuu ya Christmas, Kituo Cha Utalii wa Kiutamaduni (Serengeti Cultural Centre) kilichopo Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara kimewakosha wakazi wa mji wa Tarime ambao walipata fursa ya kupanda na kupiga picha na Mnyama Ngapmia.
Na:Binagi Media Group
Jana Siku ya Christmas na Leo Boxing Day Wananchi wengi wamefika katika Uwanja wa Mpira Sabasaba mjini Tarime na kupiga picha na mnyama ngamia na kufurahia michezo mbalimbali na mnyama (Wanyama) huo. Kama jana na leo umekosa nafasi hiyo, basi kesho jumapili ipo kwa ajili yako hivyo usithubutu kukosa.

"Hii inasaidia kukuza utalii hususani ule wa asili kwani mamia ya wakazi wa Mji wa Tarime waliofika kushuhudia michezo mbalimbali na mnyama (wanyama) huyo walifurahia zaidi hususani wakati wa kumpanda juu na kupiga nae picha". Anasema Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo hicho Joshua Nyansiri.
Ni Full Burudani
Bonyeza HAPA Kutazama Picha za Christmas Day

No comments:

Powered by Blogger.