LIVE STREAM ADS

Header Ads

TRA KAHAMA YAIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

Na Daud Magesa, KAHAMA
Mamlaka ya Mapato (TRA) Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga imepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kwa kuanza kutekeleza majukumu yake kwa kasi hadi kupelekea baadhi  ya watendaji serikalini kusimamishwa kazi  sanjari na baadhi ya sherehe za kiserikali kufutwa.

Meneja wa (TRA) wilayani humo Andrew Mgeta alisema kuwa kwa kasi hii ninatia chachu ya mabadiliko nchini ambapo hakuna nchi iliyoendelea duniani bila viongozi kujitoa katika kuwatumikia wananchi kikamilifu.

Mgeta alisema Rais kufikia kusimamisha baadhi ya watendaji serikalini akiwemo Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Rashed Bashe pamoja na kufutwa baadhi ya sherehe za kiserikali ni hali ambayo inatokana na watendaji hao kutotimiza majukumu yao japo maamuzi ya kiongozi yanayotaka kuibadili nchi yanaweza kuwafurahisha na kuwachukiza baadhi ya watu.

Aidha katika hatua nyingine Mgeta aliitaka jamii wilayani Kahama kwa ujumla kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu wake katika kuthibiti vitendo vya kitapeli vinavyofanywa na baadhi ya watu ambao si watendaji wa Mamlaka hiyo kwa kutoza kodi kwa wafanyabiashara.

Ameongeza kuwa  kuna utaratibu wa uchukuaji kodi unaotumiwa na Mamlaka hiyo na unatambulika kwa wafanyabiashara licha ya changamoto kadhaa inazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu na Utashi wa ulipaji kodi hali inyosababisha kuendesha zoezi la  kufungia baadhi ya biashara ambazo wamiliki wake wameshindwa kulipa kodi kwa wakati.

Hata hivyo Mgeta alisema mpaka sasa idadi ya maduka yaliyofungiwa na vyombo vya usafiri hususani wamiliki wake ni matajiri bado haijafahamika hadi hapo zoezi linaloendelea la kufungia maduka na kukamata vyombo vya usafiri ukomo wake utakapofikia mwezi Desemba mwaka huu.

Mamlaka Mapato (TRA) wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, imepangiwa na serikali kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 12.6  kwa mwaka wa fedha 2015/16,kulinganisha na lengo la bilioni 11.5 la mwaka 2014/ 2015.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu Meneja wa TRA wilayani humo, Andrew Mugeta, alisema wamepangiwa kukusanya kiasi cha sh Bilioni 12.6 kwa mwaka huu wa fedha, lakini hadi kufikia Oktoba mwaka huu, wamekusanya bilioni 3.97 sawa na asilimia 100 zaidi ya sh.3.96 ya malengo ya miezi hiyo.

Alisema,kama hali haitabadilika anaamini watafikia lengo walilopangiwa, la kukusanya mapato hayo ya serikali, licha ya kukabiliwa na  changamoto ya uhaba wa rasilimali ya watumishi kutokana na wilaya kupanuka.

Mugeta akizungumzia kushindwa kufikia malengo ya mwaka 2014 /15 ya kukusanya Bilioni 11.5, badala yake wakakusanya bilioni 10.6 sawa na asilimia 92 ya lengo, alisema hali hiyo ilisababishwa changamoto mbalimbali ikiwemo ya mabadiliko ya sheria hasa kwa walipa kodi wakubwa.

"Lengo la kukusanya mapato ya sh 11.5 bilioni mwaka 2014/ 15 lilikuwa kubwa, hivyo mambo kadha yaliyojitokeza ya mtikisiko wa kushuka kwa biashara  na mawalaka wa migodi, ulichangia tusifikie makusanyo kwa asilimia 8.Lakini ukiangalia kwa ujumla tulifanikiwa licha ya changamoto hizo na mabadiliko ya sheria ,"alisema Mugeta.

Alieleza kuwa, wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi kwa sababu ya kupanuka kwa wilaya, na kutokuwepo kwa utashi wa walipa kodi ,hadi wafuatwe .

"Changamoto kubwa ya walipa kodi ni ukosefu wa elimu, utashi wa kulipa kwa hiari,haupo. Low Compliance ni ndogo,hadi wafuatwe.Kutanuka kwa wilaya kusikowiana na watumishi waliopo,"alisema Mugeta.

Aidha, aliitaka jamii wilayani humo kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu wake katika kuthibiti vitendo vya kitapeli vya kuwatoza kodi wafanyabishara vinavyofanywa na baadhi ya watu ambao si watendaji wa mamlaka hiyo .

Hata hivyo,aliwahimiza wamiliki wa vyombo vya moto vya usafiri hasa pikipiki wahakikishe wanafanya usajili wa vyombo vyao kutoka namba za zamani na kupata mpya, ifikapo Desemba mwaka huu, baada y kuwa wameongezewa muda,vinginevyo vyombo vyao vitakamatwa pindi uko wa muda uliowekwa utakapofika.

No comments:

Powered by Blogger.