LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAHANGA NYANGARATA WAMEIOMBA SERIKALI KUPIGA MARUFUKU WANANCHI KUINGIA WODINI NA SIMU ZA MKONONI.

Na:Shaban Njia
Wahanga waliofukiwa katika Mgodi wa Nyangarata Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga miezi miwili iliyopita wameiomba Serikali kupiga marufuku wananchi kuingia na simu za Mikononi katika wodi za wagonjwa kwani zinawadhalilisaha wagonjwa waliolazwa.

Wahanga hao waliyasema hayo wiki hii wakati wakizungumza na katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama walipolazwa na kuongeza kuwa tangu walipofikishwa katika Hospitali hiyo kupatiwa matibabu baada ya kukaa siku 41 shimoni, watu wamekuwa wakiwapiga picha nyingi bila ridhaa yao.

Mmoja wa Wahanga hao Josephu Burule alisema kuwa tangu walipoletwa katika Hospitali hiyo kwa matibabu watumbalimbali wamekuwa wakiingia kuja kuwaona na kutumia simu zao za kiganjani katika kuwapiga picha bila ridhaa yao na kasha kuzituma katika mitandaa mbalimbal;imbali ya kijamii hali amekuwa ikiwadhalilisha.

“Tunaiomba Serikali licha ya sisi Wahanga pia Wagonjwa wenghine waliolazwa katika Mahospitali mbalimbali hapa nchini kuhakikisha kuwa inapiga marufuku watu kuingia katika wodi na simu kwani wamekuwa wakiwapiga picha wagonjwa na kisha kuzirisha katika mitandao mbalimbali”, Alisema Burule.

Aidha alisema kuwa yeye alipigwa picha na watu asiowajua waliokuja kumwona na kasha zikatumwa katika mitandao mbalimbali hali iliyowatia hofu wazazi wake walipoziona zikiwa zimekatwa vichwa na mikono na kisha kuwekwa kwa watu wengine.

“Mimi nilipigwa picha nafikiri kwa kutumia simu za kiganjani na kisha zikatumwa katika mitandao ya kijamii hali ambayo wazazi wangu walipoziona walisononeka tofauti na walivyoniona kwa macho hapa Hospitali”, Aliongeza Burule.

Hata hivyo Burule aliwataka Wasamaria wema kujitokeza katika kuwasadia kupata fedha kwa ajili ya mitaji ambayo itawasaidia katika kuanza maisha mapya watakaporuhusiwa kwani wengine majumbani kwao wameisha maliza matanga na hivyo kukosa sehemu ya kwenda.

“Mimi mwenyewe maisha yangu yalikuwa yanategemea machimbo na nilikuwa nikisaidia wazazi wangu kwa kutumia maisha hayo na kama nitakosa mtaji wa kuanzia masha pindi nikitoka Hospitali basi itanilazimu kurudi Nyangalata kuendelea na uchimbaji si wezi kukaa bila kazi kwani nitakuwa mwizi”, Alitanabaisha Burule.

Pia katika hatua nyingine Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Joseph Ngowi akizungumzia kuhusu hali za Wahnaga hao alisema kuwa wanaendelea vizuri na matibabu na muda wa siku nne zijazo wanaweza wakaruhusiwa kurudi majumbani kwao. 

No comments:

Powered by Blogger.