LIVE STREAM ADS

Header Ads

WENYEVITI SERIKALI ZA MITAA PAMOJA NA MTENDAJI WA KATA WATUNISHIANA MISURI MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
WENYEVITI watatu wa mitaa katika Kata za Nyahanga Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, wamegoma kutekeleza agizo la Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba la kuwataka kurejesha kwake mihuri wanayoitumia katika shughuli zao.

Hali hiyo ilijitokeza juzi katika kikao cha kwanza cha kujadili maendeleo ya Kata hiyo baada ya Afisa mtendaji wa Kata hiyo Yusuph Mussa kuwasilisa agizo hilo kwa wenyeviti hao ambapo hata hivyo wamelipinga vikali na kudai kuwa mtendaji huyo ameliwasilisha kinyume na utaratibu.

Wenyeviti hao ambao waliogoma kutekeleza agizo hilo Mwenyekiti wa mtaa wa Nyahanga, Supa Said (CHADEMA), Kube Shija (CHADEMA) Mwenyekiti wa mtaa wa shunu pamoja na Mwenyekiti wa mtaa wa Mtakuja, Elias Raphael.

Hata hivyo Mwenyekiti wa mtaa wa Nyahanga Supa Said alisema kuwa wao walichaguliwa na wananchi na kuanza kazi rasmi kwa kuapishwa na mwanasheria wa Halmashauri hiyo hawawezi kutekeleza agizo hilo kwa maneno bali mkurugenzi anatakiwa kuwapatia barua kwani wao Mtendaji siyo mhusika kwao.

Naye mtendaji wa Kata hiyo Raphael Mussa alisema kuwa yeye atawasilisha taarifa kwa mkurugenzi kuwa wenyeviti hao wamekaidi agizo lake hivyo achukue hatua nyingine ili waweze kukabidhi mihuri hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo Michael Magila alitoa ushauri kwa wenyeviti hao kwenda kuonana na mkurugenzi ana kwa ana ili wajiridhishe na si kumlaumu mtendaji huyo na kwamba hali hiyo itasaidia kuepusha migongano isiyokuwa natija.

No comments:

Powered by Blogger.