LIVE STREAM ADS

Header Ads

AZIKWA KABURINI NA MALI ALIZOKUWA AKIMILIKI.

Na:Shaban Njia
MTU mmoja mkazi wa Kijiji cha Mwamandi kata ya Mwanase katika halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Marashi Rutaja amefariki Dunia juzi na kuzikwa pamoja na mali zake zote alizokuwa akimiliki katika familia yake.

Marehemu Rutaja alifariki duni juzi kwa kuugua kwa muda Mrefu kabla ya kufariki Dunia alikuwa akimiliki baadhi vitu kama vile Baa pamoja na Vitu vingine katika uhai wake.

Akuzungumza na wandishi wa habari Diwani wa Kata ya Mwanase Paulo Samson alisema kuwa baada ya Wananchi wa kijji hicho kukihusisha kifo hicho na Imani ya Kishirikina waliamua kumzika Marehemu huyo pamoja na vitu vyake alivyokuwa navyo katika kaburi moja.

Alisema kuwa baadhi ya vitu alivyzikwa navyo Rutaja kuwa ni pamoja na Vitanda, Makreti ya soda pamoja na yale ya bia, Vitanda vyake  pamoja na Magodoro baada ya Wananchi wa kijiji hicho kuwa na hofu ya vitu hivyo kubaki vinaweza kuathiri kijiji pamoja na familia.

Diwani huyo alisema kuwa familia ya marehemu ilidai kuwa haiwezi kuacha kitu ahata kimoja ambacho kilikuwa kikimilikiwa na marehemu kwa hapo awali marehemu huyo alikuwa akituhumiwa vitendo vya unyanganyi katika maeneo ya kata hiyo ya mwanase.

Hata hivyo Diwani huyo aliwataka Wananchi wa kata hiyo hususani wa Kijiji cha Mwamandi kuacha kujihusisha imani mbalimbali za kishirikina kwani zinaweza zikaleta maafa katika  kata hiyo na kungeza kuwa kitendo hicho kilichofanywa na familia hiyo pamoja na Wananchi hakikuwa cha kiungwana.

No comments:

Powered by Blogger.