LIVE STREAM ADS

Header Ads

GEITA GOLD SPORT HAWAKAMATIKI KOMBE LA SHIRIKISHO.

NA OSCAR MIHAYO,Geita
Timu ya Geita Gold Sport ya Mkoani Geita imetinga hatua ya 16 bora kwa kuilaza timu ya Mgambo shooting kutoka Jijini Tanga kwa penati 4-3 kwenye mashindano ya kombe la shirikisho (FA) yanayoendelea hapa nchini.

Mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Nyakabungo sekondari mjini Geita huku Mgambo shooting ikiwa ya  ya kwanza kufunga bao kwenye dakika ya 20 kupitia kwa Bolly Shaibu kabla ya Geita kusawazisha kpitia kwa Omary Kanyoro kwenye dakika ya 41.

Mgambo shooting watajilaumu baada ya wachezaji wao Udah Sorita na Salmu Kipanga  kukosa penati na kuwafanya kuaga kwenye mashindano kwa kutolewa na timu inayocheza ligi daraja la kwanza.

Mara baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Geita Gold Sport Seleman Matola alisema kuwa siri ya ushindi ni kujituma kwa wachezaji wake kwani walijua wanacheza na timu kubwa inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara (VPL).

“Tulicheza kwa kujitambua kuwa tunacheza na timu ya ligi kuu ndo maana tumepata matokeo haya ya ushindi na hii ni salamu kwa timu tutakayokutana nayo ijiandae”, alisema Matola.

Aidha aliongeza kuwa licha ya kuwa na ushindani mkubwa wa mchezo huo timu yake inajiandaa kukutana na timu ya Polisi Tabora kwenye ligi daraja la kwanza jumamosi ya wiki hii. 

No comments:

Powered by Blogger.