LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAGU WANYAKUA UBINGWA WA MASHINDANO YA WAVU MKOANI MWANZA.

Na Oscar Mihayo Mwanza
Timu ya mpira wa wavu kutoka Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, imeibuka bingwa wa kwa seti 2-1 dhidi ya timu ya Chuo Kikuu ya Saint Augustino Kampasi ya Mwanza Saut ,kwenye bonanza lililoandaliwa na Chama Cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Mwanza katika  Uwanja wa Nyegezi Kona Jijini hapa.

Mwenyekiti wa Chama hicho juzi George Warioba alisema kuwa lengo la bonanza hili lilikuwa kuzinda kalenda ya mwaka 2016 kwani  kama chama wamejipanga kuukuza mchezo huo ikiwa pamoja na kupata uwanja wa mkoa.

Warioba alizitaja timu zilizoshiriki kuwa ni Saut, BOT, MTC, Butimba Magu zote za mkoani Mwanza, huku akiongeza kuwa Dodoma na Nzenga zilialikwa ili kuongeza ufanisi wa bonanza hilo.

Alisema licha ya kuzindua kalenda hiyo bado wanachangamoto kubwa ya ukosefu wa wafadhili pamoja na ukosefu wa uwanja wa kwao kama mkoa jambo linalosababisha kudolola kwa mchezo huo mkoani hapa.

“Bado mkoa huko kimya kwenye mpira wa wavu lakini tunajitahidi kuukuza na baada ya bonanza hii tunaanda Ligi ya Mkoa ianyotarajia kuanza kutimua vumbi April mwaka huu.

Kwa upande wake Mratibu wa Mashindano hayo Majaliwa Mayunga alisema kuwa kwa sasa watajitahidi kufuata kalenda hiyo ambayo ndani yake inamatukio 10 kwa mwaka
mzima ambao anahuakika wakiifuata wakakuwa wamepiga hatua kubwa.

Aidha aliwataka wapenzi wa mchezo huo kuwaunga mkona kwenye ligi kama kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa hamasa wachezaji na  kufanya vizuri ili kuutangaza mkoa kupitia mchezo huo.

No comments:

Powered by Blogger.