WAKAZI WA KATA YA KAYENZE MANISPAA YA ILEMELA WAKASIRISHWA NA MRADI WAO WA MAJI.
Wakazi wa Kata ya Kayenze katika
Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kukamilisha mradi wa Maji
uliopo katika Kata hiyo ili kuwanusuru na tatizo la ukosefu wa maji safi na
salama linalowakabiri kwa muda mrefu.
Wamesema kwa
miaka mingi wamekuwa wakikabiriwa na tatizo la upatikanaji wa maji katika Kata
hiyo, hali inayowalazimu kutembea umbali mrefu ili kufuata maji ya Ziwa
Victoria ambayo hata hivyo wamesema si salama kwa matumizi ya majumbani
ikilinganishwa na maji ya bomba ambayo hutibiwa kabla ya kufikishwa kwa
wananchi kwa ajili ya matumizi.
Kuhusu Mradi
wa Maji wa Kayenze uliopo katika Kata hiyo ambao chanzo chake ni maji ya Ziwa
Victoria, Wakazi hao wamesema kuwa wanasikitishwa kuona kwamba ni takribani
mwaka mmoja sasa tangu waelezwe kukamilika kwa mradi huo ambao hata hivyo wamesema
hawaoni manufaa yake.
Kilio cha Wakazi
hao kinamlazimu diwani wa Kata hiyo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM James
Katoro, kupaza sauti na kuwaahidi wapiga kura wake ya kwamba atahakikisha
anafanya kila jitihada ili kufikia mwezi wa sita mwaka huu, mradi huo uwe umeanza
kutoa maji huku pia akishughulikia suala la uchimbaji wa visima virefu katika
mitaa ya Kata hiyo ili kumaliza kabisa kero ya maji Katani hapo.
Katoro
ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara, uliofanyika jana wakati
akiwashukuru wakazi wa Kata ya Kayenze kwa kumchagua kuwa diwani wa Kata hiyo
katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana.
Bonyeza PLAY Hapa Chini Kusikiliza Zaidi.
BONYEZA HAPA KUTAZAMA PICHA
Bonyeza PLAY Hapa Chini Kusikiliza Zaidi.
No comments: