LIVE STREAM ADS

Header Ads

TARIME: Wakazi wa Kenyamanyori wakarabati barabara ya Muturu

Wakazi wa Mtaa wa Chira Kata Kenyamanyori wilayani Tarime wamefanya ukarabati wa barabara ya Muturu maarufu kama Remaghinga iliyopo Mtaa wa Buguti Kata ya Rebu ili kurahisisha magari kufika katika Mtaa wao kuchukua mawe ya ujenzi.

Zoezi hilo limefanyika Januari 02, 2016 ambapo wananchi hao walikuwa wakifanya ukarabati wa kujaza moramu katika maeneo yaliyochimbika kutokana na maji ya mvua pamoja na kuchimba mitaro kwa ajili ya kupitisha maji wakati wa mvua.

"Barabara hii imesahaulika ingawa ni muhimu kwetu kwa kuwa hapo ng'ambo kuna uchimbaji wa mawe hivyo malori huwa yanapita hapa, tumeuona tuilime ili ipitike vizuri" Amebainisha mmoja wa wakazi hao na kusema ni kawaida yao kufanya hivyo kila inapoharibika.

Hatua ya wananchi hao inapaswa kuigwa na wanajamii wengine pamoja na viongozi wenye dhamana ya kuwasimamia katika masuala ya maendeleo wakiwemo watendaji na wenyeviti wa Serikali za Mitaa kwani maendeleo yanapatikana haraka zaidi ikiwa wanajamii watashiriki ipasavyo katika shughuli za maendeleo badala ya kulalamika kuisubiri Serikali pekee.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Chira katika Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara wakishiriki zoezi la ukarabati mdogo wa barabara ya Muturu.
Hii ndiyo dhana halisi ya maendeleo.
Ni vizuri wanajamii wajiwekee utaratibu wa kutatua kero mbalimbali za maendelo katika maeneo/ mitaa yao.
Ukarabati ukiendelea.
Maendeleo yanaanza na kila mmoja katika jamii.
Maendeleo yanaanza na mimi na wewe.
Ukarabati ukiendelea.
Barabara ya Muturu (Remaghinga) ni tegemeo kwa wananchi wa kila rika wakiwemo watoto.
Mwonekano wa barabara ya Remaghinga.
Mwonekano wa baadhi ya makazi ya wananchi wanaotegemea barabara ya Muturu maarufu kama Remaghinga wilayani Tarime.

No comments:

Powered by Blogger.