LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAOMBA SERIKALI KUMCHUNGUZA MGANGA MKUU KAHAMA MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Wadau pamoja na Wafanyakazi wa Idara ya Afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama wameiomba Serikali kufanya uchunguzi kuhusu Matumizi mabaya ya Mali za umma pamoja na utendaji kazi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ana matumizi mabaya ya Madaraka kwa wafanyakazi.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu uligundua kuwa Mganga  huyo Bruno Minja  amekuwa na matumzi mabaya ya Madaraka hasa kwa Wafanyakazi wa Idara ikiwa ni pamoja na kutumia mali za umma katika shughuli zake binafsi kama vile magari ya Serikali kusomba vifaa vya ujenzi.

Mganga Mkuu huyo pia anatuhumiwa na Wafanyakazi katika kitendo cha kuwagawa huku akitumia zaidi ukabila hali ambayo imeleta Mpasuko mkubwa na makundi na hivyo kufanya utendaji wa kazi katika Hospitali hiyo kuwa wa hali ya chini kuliko ilivyokuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Idara hiyo walisema kuwa Mganga Mkuu huyo ambaye ana kipindi cha miezi sita tangu ahamie katika Hospitali hiyo amekuwa akituhumiwa katika masuala ya kuwanyima Wafanya kazi stahiki zao za msingi kama vile fedha kwa ajili ya masaa ya ziada ya kazi yanapotokea katika Hospitali.

“Mimi nikuwa ni Dereva katika Hospitali hii na siku moja Mganga Mkuu aliniagiza kwenda Jijini Mwanza kwa ajili ya kumbebea vifaa vya ujenzi nikiwa na gari ya Serikali na nilipomwomba Posho kwa ajili ya Safari alikataa na kuchukua hatua za kunitoa katika kitengo cha Udereva”, Alisema mmoja wa Madereva katika Hospitali hiyo.

Mganga Mkuu huyo alipotafutwa kujibu thuma hizo alikanusha vikali na kuongeza kuwa yeye hausiki na tuhuma hata moja katika Hospitali na kungeza kuwa hayo yote ni majungu na kundi moja ambali halizidi watu sita ambalo limedhamiria kumchafua katika utendaji wa kazi wake.

“Ndugu Mwandishi wa Habari hapa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa  Kahama kuna majungu na kundi dogo ambalo kutokana na kuziba mianya yao ya kuta maslahi katika Hospitali hiyo na kuwahamisha katika vituo vya nje  ndio wameamua kuchukua jukumu la kunichafua na mimi kimsingi sitaacha kuwafutilia katika utendaji wao wa kazi”,Alisema Bruno Minja.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba akiongelea kuhusu suala hilo alisema kuwa yeye amelisikia juujuu na hivyo kuomba muda kwa ajili ya kulifanyia kazi suala hilo na majibu yakipatikana angweza kulitolea ufafanuzi katika vyombo vya habari.

No comments:

Powered by Blogger.