LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATEJA "KUWASA" WATAKIWA KUWA MAKINI NA MAFUNDI WANAOMBA RUSHWA.

Na:Shaban Njia
WATEJA wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Wilayani Kahama Mkoni Shinyanga "KUWASA" wametakiwa kuwa makini katika kupatiwa huduma za uunganishiwaji maji zinazotolewa na baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kutokana na vitendo vya rushwa vilivyokithiri kwa  mafundi wa Idara  hiyo.

Hayo yalibainishwa na Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Wilaya Kahama (KUWASA) Joel Rugemalira wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake kuhusu ufafanuzi wa baadhi ya Wateja wa mamlaka yake kulalamika juu ya vitendo vya rushwa kukithiri kwa baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.

Rugemalira alisema kuwa kuna baadhi ya Wafanyakazi katika Ofisi yake hawafuati maadili ya utumishi wa umma ukiwa ni sambamba na kupokea Rushwa kutoka kwa Wateja wanaotaka kupata huduma ya kuunganishiwa maji katika nyumba zao kinume cha Sheria.

“Katika Ofisi yangu tayari hadi kufikia hivi sasa kuna baadhi ya Wafanyakazi tumeshawafukuza kazi kutokana na sababu kama hizo na bado zoezi hili litaendelea kwa watumishi ambao hawatakuwa na maadili ya utumishi wa umma katika ofisi yangu”, Alisema Joel Rugemarila

Rugemarila aliwaomba Wateja hao kuhakikisha kuwa wakilipia huduma ya kuunganishiwa maji wahakikishe kuwa wanapatiwa Stakabadhi(LISTI) ambayo itakuwa ni ushahidi mkubwa pindi matatizo yeyote ya kuhusu kuunganishiwa maji yanapotokea katika ofisi yake hasa katika masuala ya Rushwa.

“Ninawaomba Wateja wangu lipieni huma za kuunganishiwa maji katika ofisi husika na acheni kulipia maitaani na kuhakikisha kuwa mnapatiwa stakabadhi katika dirisha lilipo mahususi mkwa ajili ya kulipia katika ofisi ya idara ya maji iliyopo mjini Kahama”, Alisema Meneja huyo.

Aidha Meneja huyo alisema kuwa hana malalamiko yeyote yaliletwa katika ofisiyake kuhusu huduma za uunganishiwaji wa maji kutoka kwea wateja ilia amekuwa akipata malalamiko mengi ambayo yamekuwa hayaji katika maandishi hali ambayo inamafanya kuyachukulia kama majungu na kutoyafanyia kazi kwa wakati.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo John Mkama alisema kuwa katika Mamlaka hiyo kuna matatizo makubwa ya Watumishi kuvamia katika Idara ambazo hawakupangiwa kufanyiwa kazi hali ambayo inafanya baadhi ya idara kukosa watumishi kwa kuwa tayari wameenda katika sehemu nyingine ambazo sio kazi zao mahususi.

“Katika idara hii vitendo vya rushwa vinalipotiwa hasa na wateja,maana kuna wafanyakazi wa idara hii wanajifanya kuwa ni mafundi huku hawana fani hiyo na ndio maana wateja wanawapatia fedha hizo ili wawaunganishie maji haraka huku mfanyakzi huyo hana uwezo wa kumfungia maji maana sio fani yake”,alisema Afisa Mahusiano John Mkama

Pia Mkama alisema kuwa kwa sasa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazinigira katika Halmashauri ya Mji wa Kahama inakabiliwa na Changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kuwaji wa haraka wa Maji hali ambayo maeneo yameongezeka na hivyo kufanya wateja wapya kuwa wengi kuliko huma za maji zinazotolewa katika mamlaka hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.