LIVE STREAM ADS

Header Ads

AKAMATWA NA KETE MBILI ZA DAWA YA KULEVYA MJINI KAHAMA.

Na:Shaban Njia
JESHI la Polisi Mkoani Shinyanga linamshikilia Said Abbakari (37)mkazi wa mtaa wa malunga kata ya Malunga wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa kosa la kukutwa na kete mbili za madawa ya kulevya pamoja na Bangi.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Mika Nyange akizungumza na gazeti hili alisema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juzi baada ya jeshi la Polisi wilayani Kahama kuizunguka nyumba ya mtuhumiwa huyo  ndipo walifanikiwa kumnasa.

Kamanda Nyange alilieleza kuwa Abbakari anashikiliwa kwa kosa la kukutwa na kete mbili za madawa ya kulevya aina ya MANDRAC pamoja bangi na kuongeza kuwa nimuuzaji maarufu wa madawa hayo mjini Kahama.

“Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa kwa wasamaria wema lilianza siku nyingi kumsaka mtuhumiwa huyo bila mafanikio ndipo usiku wa kuamkia juzi Februari 26 baada ya jeshi la Polisi kuzingira nyumba yake tulifanikiwa kumkamata.

“Alikutwa na kete mbili za madawa ya kulevya aina ya Mandrac pamoja na Bangi lakini pia anadaiwa kuwa pembezoni mwa Hospital ya Mji wa Kahama wanapotengenezea Majeneza anakijiwe chenye kundi kubwa la vijana wanauza madawa hayo.

Nyange aliesema kuwa katika makundi hayo wapo watuhumiwa wengine wakijifanya ni mafundi wa Majeneza pengine mafundi hao nao pia ni wateja wake”,alisema Kamanda Nyange.

Hata hivyo Nyange alisema kuwa kutokana na hali hiyo mnamo februari 29,mwaka huu mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma hizo zinazomkabili huku upelelezi ukiendelea wa kuwasaka wenzake na kwamba kupitia mtuhumiwa huyo wataweza kuwabaini walio juu yake.

“Abbakari ni muuza madawa sugu ya kulevya na ni maarufu kwa Wilaya ya Kahama sana kwa kazi hiyo na aliposakwa alikuwa akijificha na jeshi la polisi litahakikisha linawasaka na kuwatia mbaloni vijana wake wote wanaodaiwa kufanya naye kazi hasa hapo kwenye kijiwe cha majeneza,”aliongeza Kamanda Nyange.

Alisema jeshi la Polisi litaendesha msako mkali wa kuwabaini wanaojihusisha na shughuli hiyo katika Mkoa Shinyanga hususani katika vijiwe mbalimbali vya Shunu,Mashine za mpunga Kahama, Shule ya msingi Kilima,Daraja la kuelekea Ndara(Upongoji) Ibinza,mata pamoja na Ngokolo.

Katika mkoa wa Shinyanga hususani Wilaya ya Kahama kumezuka wimbi la kiharifu(VIBAKA) linalohusisha vijana wadogo walio chini ya umri wa miaka 18 walio  katika makundi ya uvutaji madawa ya kulevya na bangi.

No comments:

Powered by Blogger.