LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANAHABARI WA STORM FM YA MKOANI GEITA, JOEL MADUKA AMVISHA PETE YA UCHUMBA BI.DEBORA JACKSON.

Mtangazaji na Mwanahahabari wa Storm Fm ya Mkoani Geita, JOEL MADUKA (Kulia) ambae ni Mkazi wa Jiji la Mwanza, leo February 28,2016 amemvisha Pete ya Uchumba na kumtambulisha rasmi Mchumba wake DeEBORA JACKSON ambae ni Mkazi wa Lumala, Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, mbele ya Viongozi wa dini, Waumini pamoja na Wanafamilia.

Shughuli hiyo imefanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, katika Ibada iliyoongozwa na Mchungaji wa Kanisa hilo Mch.Daniel Kulola.
Mipango ya harusi inafuata na wawili hao wanatarajia kufunga pingu za maisha Wikendi ijayo. 

Kulia ni Joel akimtambulisha na kuelezea sifa za Mchumba wake mbele ya waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Ilemela Mkoani Mwanza.
Bibi harusi Mtarajiwa Debora Jackson (Kushoto) akimtambulisha na kuelezea Sifa za Bwana harusi Mtarajiwa Joel Maduka mbele ya waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Manispaa ya Ilemela hii leo.
Baada ya utambulisho, Bi harusi mtarajiwa akimzawadia mchumba wake zawadi ya perfume ishara ya upendo
Katikati ni Mchungaji Daniel Kolola akiwaonyesha waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya pete iliyoandaliwa na Bwana Harusi Mtarajiwa, Joel Maduka kwa ajili ya kumvisha Bi harusi Mtarajiwa.
Joel Maduka (Kulia) akimvisha Mchumba wake Debora Jackson Pete ya Uchumba mbele ya waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Ilemela Mkoani Mwanza.
Joel Maduka akimpendezesha Mchumba wake kwa kumvalisha viatu alivyomzawadia
Bi harusi Mtarajiwa, Debora Jackson akionyesha Pete ya Uchumba aliyovishwa na Mchumba wake Joel Maduka
Viongozi wa Dini wakiwaombea Maharusi watarajiwa
Kulia ni Mchungaji Daniel Kolola akiwatambulisha Wanandoa watarajiwa mbele ya Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Ilemela Mkoani Mwanza.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Ilemela Mkoani Mwanza wakifuatilia ibada ya utambulisho wa Uchumba katika Joel Maduka na Debora Jackson
Joel Maduka (Kushoto) akiwa pamoja na Mchumba wake Debora Jackson (Kulia).
Wanafamilia upande wa Bibi Harusi wakiwa na Wanandoa watarajiwa
Wanafamilia Upande wa Bwanaharusi wakiwa pamoja na Wanandoa watarajiwa
Bwana harusi Mtarajiwa (Katikati) akiwa pamoja Wanafamilia
Maharusi watarajiwa wakilishana Msosi Ishara ya Upendo
Maakuli kama kawaida
Cheers Kama kawaida
Picha ya Pamoja ya Wanafamilia wa Pande zote mbili za Maharusi watarajiwa.
Dada wa bwana harusi (Kushoto) akitoa wosia wake
Maharusi watarajiwa wakiwa katika Karanga Photoo na Kamera ya BMG.
Imeandaliwa na Binagi Media Group-BMG.

No comments:

Powered by Blogger.