WALIMU NYASUBI WAOMBA SERIKALI KUONGEZA RUZUKU MASHULENI ILI KUKABILIANA NA SERA YA ELIMU BURE
Na:Shaban Njia
Waalimu na Wanafunzi katika Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga, wameiomba Serikali kuongeza Ruzuku mashuleni ili kukabiliana na matatizo mbalimbali kama vile upungufu wa Madawati pamoja na Ujenzi wa Madarasa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nyasubi Mjini Kahama Mpena Musa, anasema kuwa kwa sasa sera ya Elimu bure iliyotolewa na Rais John Magufuli imechangia kwa kiasi kikubwa kwa Wazazi kujitokeza katika kuwaleta wanafunzi shule.
Anasema kuwa kutokana na mwamko huo wa wazazi umechangia baadhi ya shule kupata wananfunzi wengi kuliko walivyotarajiwa hali ambayo imefanya kuwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya Madarasa katika shule husika.
Aidha Mwalimu Mkuu huyo anasema kuwa katika shule yake ya Nyusubi jumla ya Wananfuzi 560 waliofaulu darasa la saba katika kipindi kilichopita walipangiwa kujiunga na shule hiyo hali ambayo imefanya kuwa na mbanano mkuwa katika madarasa kwani yapo madarasa matatu tuu.

“Tunaiomba Serikali angalau iongeze fedha mashuleni kama Ruzuku kwani kwa sasa huwezi kumchangia mzazi mchango wowote katika shule kutokana na sera ya Rais wetu ya elimu bure kutoka chekechea hadi sekondari na katika shule yangu kuna upungufu wa madarasa 11 huku Halmashauri ya Mji ikihaidi kujenga madarasa mawili kati ya hayo”, Alisema Mwalimu Mpena Musa.
Aidha katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakato kata ya Nyasubi Wilayani hapa Mayunga Alphonce amewataka baadhi ya wafanyabiashara mji hapa kujitokeza katika kusaidia miche ya miti katika sekondari ya Nyasubi kwa lengo la kuiotesha na kuwasadia wanafunzi kupata kivuli wakati wa mapumziko.
Mayunga ameyasema hayo wakati wa zoezi la upandaji wa miti 300 katika sekondari hiyo lililofanywa na Wanafunzi wa kidato cha kwanza ambayo ilitolewa na baadhi ya wafanyabiashara wa miti waliopo pembezoni mwa barabara kuu katika Kata Nyasubi eneo la Mtaa wa Nyakato mjini Kahama.
Anasema kuwa Shule ya Sekondari ya Nyasubi kwa sasa haina miti wala kivuli chochote hali ambayo imekuwa ikisababisha Wanafunzi kukosa maeneo ya kupumzika hasa nyakati za Mapumziko wawapo Shuleni.
“Ninawaomba Wafanyabiara kutuisadia miti ya kivuli katika shule yetu kwani kwa sasa tunapata taabu Walimu na Wanafunzi kupata sehemu za kupumzikia kutokana na ukosefu wa miti na hivyo kufanya shule kuwa kama katika jangwa”, Alisema Mwenyekiti huyo wa Mtaa.
Aidha Mayunga anaendelea kusema kuwa hata wangepata miti ya matunda mbalimbali kama vile machungwa pia ingewza kusadia katika kipindi kijacho katika kuwasaidia Wanafunzi kupata lishe kwa kutumia matunda hayo na kuongeza ufanisi katika masomo yao kisaikojia.

No comments: