WATANZANIA WAMLILIA MWANAHABARI FRED MOSHA.
Fred Mosha,mbona umelala
mapema?tungekuwa na uwezo tungekumsha kama alivyoamshwa Lazaro,lakini hilo
hatuliwezi,lala Fred,pumzika Fred Mosha,mtoto wako,mkeo,wazazi,dada na
kaka,pamoja na wadogo zako wanakulilia,wana SAUT wenzako wanakulilia,wana
Tumaini Media wenzako wanakulilia,wana Arsenal na Yanga wenzako
wanakulilia,rafiki zako mitandaoni wanakulilia,uliosoma nao shule ya msingi
mpaka sekondari wanakulilia,jirani zako wanakulilia,ndugu,jamaa na marafiki
wanakulilia,nami rafiki yako ninakulilia FRED MOSHA,mwandishi na mtangazaji wa
habari wa Redio TUMAINI uliyetutoka leo asubuhi.
Fred,mamia
kwa maelfu tunakulilia kwa sababu ya moyo wako,upendo,huruma na vipaji
ulivyokuwa navyo ambavyo sasa tutavikosa kutoka kwako,Fred nakulilia sababau
bado nakumbuka jinsi tulivyokuwa marafiki tangu tufahamiane hapo mwaka 2003
tulipokutana Chuo Kikuu wakati tukiwa wanafunzi,leo Fred
umelala,hupumui,usemi,hucheki kama ilivyokawaida,nakuita seneta,jina
nililopenda kukuita huitiki,nakulilia Fred.
Fred
umeacha mtoto mdogo aliyependa sana kukua katika malezi yako,umemuacha mkeo
ambaye wewe ulikuwa ni mhimili mkubwa kwake,umeicha Redio TUMAINI ambayo wewe
ulikuwa mhimili mkubwa sana pale,nakulilia Fred.
Fred
ukiwa mwafunzi chuo kikuu ,ulikuwa zaidi ya mwanachuo,wewe ulikuwa ni mwalimu
kwenye madarasa ya usomaji wa habari,kwenye postmortem,waandishi wengi wanakulilia,mchango
wako kwa waandishi wanaotamba na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi
naukumbuka mpaka leo,ndiyo maana nakulilia,nakumbuka jinsi ulivyokuwa ukimuita
na kumtia moyo Lizzy Masinga ambaye kwa sasa yupo na BBC ukimtania na
kumwambia,”WEWE NI BONGE LA MTANGAZAJI”leo LIZZY ni mtangazaji kinara wa
BBC,ulitabiri hilo Lizzy akiwa mwanafunzi.Ndiyo maana nakulilia Fred.
Nakumbuka
jinsi ulivyokuwa unatangaza kipindi cha Morning Pressure cha Radio SAUT na
Michael Baruti ambaye sasa yupo na BBC,nakumbuka ulivyoniambia DOTTO ,NOEL
THOMSON ambye kwa sasa yupo na BBC kuwa ni mtangazaji mzuri sana,nakumbuka
ulivyokuwa unatangaza kipindi cha Kwasakwetu cha Redio SAUT na Bernard James wa
Star TV,Nakumbuka jinsi ulivyokuwa unamtia moyo Sabina Nabingambo ambaye kwa
sasa yupo na RFI,naukumbuka utani wako na LEAH MUSHI wa TBC ,Cesilia Ndabigene
wa Tumaini Media kwa sasa wakati mkiwa redio SAUT FM.Ndiyo nana nakulilia Fred.
Nakumbuka
jinsi ulivyokuwa kiongozi wa dawati la michezo la Radio SAUT,uliibua vipaji vya
watangazaji wa kike,ni wewe ulianzisha utaratibu wa rdio SAUT FM kuhoji
sources,naikumbuka siku ulipopiga simu kwa Frolian Kaijage wakati akiwa msemaji
wa TFF ,kipindi Taifa Stars ikiwa Ivory Coast,watu wakasema sasa SAUT RADIO ni
level nyingine,nakumbuka Michael Barudi ambaye sasa yupo na BBC wakati akiwa
bado SAUT alinifuata usiku wakati akija kufanya kipindi cha FRIDAY BANG,na
kuniambia “hiki walichofanya akina Fred na Wakuganda,ni level nyingine”,Ndiyo
maana nakulila Fred.
Nakumbuka
jinsi ulivyokuwa hukosekani kwenye vipindi vya Ya kale ni dhahabu,Anga za
michezo,kwasa kwetu,Morning Pressure na taarifa za habari,ulikuwa ndiyo
mtangazaji kinara wa redio SAUT,leo haupo,naukumbuka utani wako na Renatusi
Sona na Josephat Mwanza,Liberatus Chonya.adeline Kaijage,Domina Rwemanyira,Rich
Ngaiza,Darius Mukiza,Johh Livet,Anikazi Kumbemba.Audifax Kamala,Emmanuel
Mbando,Clecence Kunambi,Robert Hokololo,Joyce Mgaya,Zuhura Mwera,Harrison
Kisaka,Protas Lubaba.n.k
Mara
nyingi ulikuwa unawatia moyo wanafunzi wenzako wawekeze kwenye vitendo huko
ukiwaatia orodha ya watangazaji na waandishi nguli,uliamua kubandika kwenye
ukuta wa redio SAUT majina ya watangazaji waliopita hapo na sasa ni magwiji ili
vijana wadogo wapate mwamko,ulibadika majina ya akina Grace Kagobo(DW).Zawadi
Machibwa(BBC),Upendo Wella,Gervas Hubire,Charles Mwebeya,Festus
Mwakelubi,Joselyne Kitakwa,Anna Kwambaza,Fatuma Matulanga(TBC),Jonas
Songora(Radio JAPAN),Lazaro Matalange na wengine wengi kama njia ya kuwapa
hamasa wanafunzi kuwa wanaweza fika mbali.Ndiyo maana nakulilia Fred.
Fred
ulikuwa mwelevu,mpole,mwenye huruma siku zote,ulipenda wanafunzi wenzako
wafanikiwe,na hili nililiona wakati tukifanya Postmortem SAUT,ndiyo maana
nakulilia Fred.Fred ukiwa Tumaini Media,ulijikusanyia mashabiki wengi,ulikuwa gwiji
kwenye muziki wa dansi,kongo na muziki wa zamani,ulikuwa gwiji kwenye sports na
usomaji wa taarifa za habari,leo umetangulia Fred,Ndiyo maana nakulilia.
Nashindwa
nichague yapi ya kukuelezea Fred,yako ni mengi yanahitaji kitabu na siyo
ukurasa wa FB,,nabaki nakulilia Fred Mosha,nilipenda kukuita SENETA,kamsalimie
rafifi yangu EDSON KAMUKARA,nitawakumbuka sana,EDSON aliniliza sana,leo FRED
unaniliza zaidi,nawakumbuka sana,mlikuwa msaada wangu wakati mkiwa wanafunzi
SAUT,Tanguli Fred Mosha,Tangulia Fred,umeteseka sana katika ugonjwa,vita
umevipiganasafari umeimaliza,Tangulia Fred Mosha,kamsalimia Nkwabi
Ng’wanakilala.
Na:Dotto Bulendu
No comments: