LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATUMIAJI WA SIMU JIJINI MWANZA WAIPONGEZA MAMLAKA YA MAWASILIANO NCHINI TCRA.


Baadhi ya Watumiaji wa Simu za Mkononi Jijini Mwanza, Wameupongeza uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wa kusitisha Matumizi ya Simu bandia ifikapo mwezi June Mwaka huu.

Pongezi hizo zimejiri ikiwa ni siku chache baada ya TCRA kutangaza kuzifungia Simu za Mkononi ambazo ni bandia au Fake kama ambavyo zinafahamika zaidi kwa lugha ya kigeni na kuongeza kuwa hatua hiyo itawasaidia kujiepusha na madhara anayoweza kuyapata mtumiaji wa simu fake ambayo ni pamoja na kuathiri uwezo wa kusikia unaotokana na mionzi mikali ya simu hizo.

Licha ya TCRA kupewa pongezi hizo, baadhi ya Wanachi Jijini Mwanza, wamehoji ni kwa nini simu hizo zimekuwa zikiruhusiwa kuingizwa nchini huku wakiongeza kuwa mpango huo utawaathiri watumiaji wa simu walio wengi hapa nchini.

Mkakati wa kufunga Matumizi ya Simu Fake nchini, pia umethibitishwa na Injinia Lawi Odielo ambae ni Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa , ambae ametanabaisha kwamba utekelezaji wake utaanza kuanzia June 17 Mwaka huu, ambapo amewataka watumiaji wa Simu kuthibisha mapema ikiwa simu zao ni Orginal ama feki.

Ili kuthibitisha ikiwa simu yako ni Orginal, unapaswa kupiga *#06# na utapata Serial namba ambazo utazituma kwenda nambari 15090 na utapokea ujumbe mfupi wa maneno kuwa simu yako ni Orginal au Fake.
BONYEZA HAPA Kusikiliza  Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.

No comments:

Powered by Blogger.