LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAASISI YA INTERNATIONAL LANGUAGE TRAINING CENTRE SASA INAPATIKANA ISAMILO JIJINI MWANZA.

Charles Mombeki ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kufundisha Lugha mbalimbali Jijini Mwanza, International Language Training Centre.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Kutokana na Mwitikio mkubwa wa Watanzania kujifunza lugha mbalimbali za Kimataifa ikiwemo Kiingereza, Taasisi ya Kufundisha Lugha ya International Language Training Centre imeamua kuboresha wigo wa huduma zake baada ya kuhamia katika eneo jipya na bora lililopo Isamilo Jijini Mwanza.

"Tumehamia hapa (Isamilo) kutoka Mtaa wa Balewa ikiwa ni katika juhudi za kuendelea kuboresha huduma zetu ambapo huku (Isamilo) tumepata eneo kubwa ambalo linatuwezesha kutoa huduma bora za Masomo pamoja na Internaten bure. Amesema Charles Mombe ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ambayo pia inatoa huduma ya Malezi ya Watoto (Day Care) pamoja na Mafunzo ya Kompyuta.

Taasisi ya International Language Training Centre inayopatikana Isamilo Jijini Mwanza jirani na Ofisi za Medical Research, hufundisha lugha mbalimbali za Kitaifa ikiwemo Kiswahili na Kisukuma pamoja na lugha za Kimataifa ambazo ni pamoja na Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kijapani na Kichina kwa lengo la kuwaandaa wahitaji wake kukabiliana na ushindani wa mwingiliano wa mataifa mbalimbali duniani.
Bonyeza HAPA Kwa Kujua Zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.