LIVE STREAM ADS

Header Ads

BALAA NYAMANORO JIJINI MWANZA. AKUTWA AKIONYESHA PICHA ZA NGONO NA KISHA KUCHEZA MCHEZO MCHAFU.


Judith Ferdinand, Mwanza
Uongozi wa Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, umebaini ukumbi unaonesha   mikanda ya  video   za ngono , kwa watoto chini ya umri wa miaka 18  nyakati asubuhi.

Hii imebanika kutokana na oparesheni  inayoendelea  katika kata hiyo, ya kuhakikisha baadhi ya biashara na michezo  haifanyiki asubuhi  ikiwemo  pool, kahawa, bar pamoja na kumbi za video, ikiwa ni utekelezaji wa agizo kutoka serikali kuu kupitia rais Magufuli.

Akizungumza ofisini kwake  jana, Ofisa Mtendaji wa  kata hiyo, Nhikilo Elias alisema,  wakati wakiendelea na oparesheni hiyo siku ya ijumaa, walipata  taarifa kutoka kwa wananchi  wa  mtaa wa Nenetwa juu ya kuwepo  ukumbi  video  unaoonesha  mikanda ya ngono kwa watoto  wa kiume walio chini ya miaka 18   wakati wa asubuhi muda wanaotakiwa kuwa shuleni.

Elias alisema licha ya kuonyesha mikanda hiyo kumekuwa na tabia ya  muhusika  wa ukumbi huo aliyejitambulisha  kwa jina la Rashid Juma kuwalazimisha watoto hao  kumuingilia kinyume na maumbile ( kumlawiti), jambo ambalo ni hatari kwa afya zao sambamba kuathirika  kisaikolojia na kupelekea kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.

Pia alisema,aliwaagiza  watendaji wa kata hiyo akiwemo Ofisa Ustawi wa kata , kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha katika ofisi yake , na kufanya mahojihano na muhusika  pamoja na baadhi ya wanafunzi  waliokutwa wakiwa pamoja naye katika ukumbi huo wakati masomo yakiendelea  shuleni, mtuhumiwa huyo  alipelekwa kituo cha polisi kwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii wa kata hiyo, Deograsia Lubungo alisema, aliletewa  taarifa hiyo jana na wanafunzi wawili wakiwa wameongozana na  wakinamama wawili ambao walisema kuwa kuna wanafunzi wenzao wapo katika ukumbu huo usiokuwa na jina,  wanaangalia mikanda ya ngono pia hulazimishwa kumuingilia  kinyume na maumbile  mtuhumiwa huyo.

Hivyo walivyofika  eneo la tukio  walimkuta muhusika akiwa na wanafunzi hao, huku   televisheni  inazimwa  ikimaanisha kuna kitu walikua wanaangalia muda uliopita , pia ndani ya ukumbi huo kuna chumba chenye  godoro kinachosadikiwa  kutumika  kufanya mchezo huo sambamba na kukamata cd na flash.

Mmoja wa watoto ambao walikutwa katika ukumbi huo wakiwa na mtuhumiwa Abubakali Aprodus  alikiri,  kuwahi kumuingilia kinyume na maumbile mtuhumiwa huyo  baada ya kumlazimisha,   na kusema  kuwa amekuwa akiwarubuni  kutoroka shule na kuwawekea mikanda ya  video za ngono  kwa ajili yakukidhi haja zake binafsi.

Kwa upande wake mmoja wa wazazi wa watoto hao  Baby Abdalah alisema, kuwa kitendo alichofanya mtuhumiwa huyo ni ukatilii, hivyo anaiomba serikali kumchukulia hatua za kisheria, ili iwe fundisho kwa wengine, pamoja na wanafunzi hao kupimwa afya na kuelimishwa juu ya athari zitokanazo na ufanyaji mchezo huo.

Naye mmoja wa shuhuda wa tukio hilo  Fredrick Patrick alisema, mtuhumiwa huyo amewai kukanywa na wazazi wake kuhusu kujiusisha na vitendo hivyo lakini hakusikia, hivyo anaiomba serikali itoe adhabu kali endapo atabainika  na kosa, hili liwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia kama hiyo. 

Hata hivyo kwa upande wake mtuhumiwa huyo Rashidi Juma, alikana kujihusisha na uonyeshaji video za ngono sambamba na kuwalazimisha watoto kumuingilia kinyume na maumbile, bali alisema kuwa hizo ni tuhuma tu ambazo haelewi chanzo chake.

Aidha Mwenyekiti wa mtaa wa Nenetwa Lucas Rwechungula alisema, jambo alilofanya mtuhumiwa ni kinyume na maadili ya nchi, hivyo anoomba chombo husika kusimamia sheria na akibainika anamakosa apewe dhabu kali, itakayopelekea wengine kuogop kuendelea kufanya vitendo kama hivyo.

Pia aliiomba jamii kuendelea kufichua vitendo vya kikatili vinavyoendelea katika maeneo yetu, pamoja na wazazi kufatilia maendeleo ya mtoto shuleni ili kuepuka utoro unaosababisha kuingia katika mikono ya watu wabaya kama ya mtuhumiwa.

No comments:

Powered by Blogger.