LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI BULUNGWA WAJITOLEA KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO.

Na:Shaban Njia
KUFUATIA Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Isabela Chilumba kudai kuwa hana bajeti ya ujenzi wa wodi ya akinamama na watoto katika kituo cha afya cha Bulungwa,wananchi wa kata hiyo wameibuka na kichanga kiasi cha mifuko 100 ya saruji kwa ajili wa ujenzi huo.

Diwani wa kata ya Bulungwa Joseph Masaluta, aliyasema hayo  juzi wakati akielezea masikitiko yake kwa mkurugenzi huyo kutojenga wodi hiyo ya akinamama na watoto kwani katika wodi moja iliyopo wanachanganywa watoto,wanaume pamoja na akinamama kwakulazwa chumba kimoja cha wodi.

Masaluta alisema kuwa kitendo chakuwa na mchanganyiko huo huduma mbalimbali zinashindikana kufanyika zikiwemo kama za uchomaji wa sindano ikiwemo ubadilishaji wa nguo hasa wakinamama kutokana na kukutanishwa katika chumba kimoja huku wakiwa jinsia tofauti wanaume, wanawake pamoja na watoto.

Alisema kuwa kutokana na tatizo hilo kupitia vyama vya msingi vya tumbaku vya Tembo,Ibuka pamoja na Mweli vilivyopo katika kata ya Bulungwa wameamua kuchangishana fedha na kufanikiwa kununua mifuko ya saruji 100 itakayosaidia katika unzishwaji wa ujenzi bila kutegemea fedha kutoka halmashauri.

Hata hivyo Msaluta alisema changamoto kubwa inayoawakuta wananchi wa kata hiyo  ni kukosekana kwa mashine ya kufyatulia tofari ambayo ipo katika kata jirani ya Nyamilangano nakuongeza kuwa kama itapatikana kwa wakati ujenzi wa wodi hiyo utaanza mara moja kwa nguvu ya wananchi.

Hata hivyo diwani huyo alisema kuwa changamoto nyingine ni kukuosekana kwa chumba cha kuhifadhia maiti hali ambayo maiti hulazimika kuachwa katika kitanda alichokuwa amelazwa,nakuongeza kuwa ndugu wa marehem kama yupo mbali inawapa woga wagonjwa wengine kutokana na maiti kuachwa kwa mda mrefu kitandani.

Kutokana na hali hiyo diwani huyo alisema kuwa anaiomba serikali kutochelewa kutoa fedha za maendeleo katika kata,nakungeza kuwa kucheleweshwa kwa fedha hizo kunaweza kusababisha madhara makubwa kwa wananchi kwa hawapati huduma za kijamii kwa wakati mwafaka.

Katika kikao cha baraza la Madiwani kilichokaa mwaka jana,Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu Isabela Chilumba alikaririiwa na vyomba vya habari akijibu swali la diwani wakata ya Bulungwa Joseph Masaluta akitaka kujua kama Halmashauri yake imetenga fedha kwa ajiri ya ujenzi ya wodi ya akinamama na watoto pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti.

Katika kikao hicho Mkurugenzi huyo akitoa majibu,alisema kuwa Halmashauri yake kwa kipindi cha mwaka wa fedha haijapanga kujenga wodi ya akinamama na watoto pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti na kumtaka Diwani huyo asubili hadi bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

No comments:

Powered by Blogger.