LIVE STREAM ADS

Header Ads

JUMUIYA YA WANAWAKE SHINYANGA YAMPONGEZA MAGUFULI KWA KUFUATA UTAWALA BORA.

Na:Shaban Njia
JUMUIA ya Wanawake ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga (UWT) imempongeza Rais wa awamu ya Tano Dr, John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kuhakikisha kuwa watumishi wa Serikali yake wanafanya kazi kwa kufuata weledi pamoja na utawala Bora.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Katubu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Josephine Nyengu wakati akisoma taarifa ya Jumuia hiyo mbele ya Mgeni Rasmi katika sherehe za kuazimisha miaka 39 ya Chama cha Mapindzi zilizofanyika katika Kata ya Nyamilangano Wilayani Ushetu.

Nyengu alisema kuwa Umoja huo unatambua mchango mkubwa ulioletwa na Rais Magufuli katika utawala wake ikiwa ni sambamba na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali katika taasisi zake hapa Nchini.

Pia Jumuia hiyo ilimpongeza Rais Magufuli kwa kuteuliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa umoja wa Nchi za Afrika Mashariki ikiunganisha nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda pamoja na Kenya.

Aidha alisema kuwa Jumuia yake inaunga Mkono  timu nzima ya utendaji kazi wa Rais Magufuli katika kutekeleza masuala yote ya maendeleo ikiwa sambamba na kuimarisha utawala bora na kusimamia ipasavyo rasilimali za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizunguzia Changamoto zinazoikabili Jumuia hiyo Katibu huyo wa UWT Mkoa wa Shinyanga alisema kuwa wanakabiliwa na ukosefu wa Vyanzo vya mapato hali ambayo inachangia kushindwa kuchangia katika masuala mazima ya Elimu, afya na maji katika Mkoa wa Shinyanga.

Nae Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Angela Paulo aliwataka Wazazi wasiwe na tama ya kuchukua mahali za kuwaozesha watoto na kuongeza kuwa kwa kuwaozesha watoto mapema kunawandolea haki yao ya msingi ya kupata Elimu kwa wakati na kuwakwamisha kutimiza ndoto zao.

“Ninawaomba wazazi kuacha kuwa na tama ya kutaka utajiri kwa kupitia watoto wanaosoma natoa angalizo kwa watu wa namna hiyo tutawachulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria”, Alisema Angela Paul.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika sherehe hizo Mbunge wa Jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa alisema kuwa ni lazima kwa sasa Wanachama wa Jumuia hiyo waunganike pamoja na ili kuleta maendeleoa katika uongozi wa ngazi za chini ambapo ndipo kwenye shina.

Pia aliitaka Jumuia hiyo kuunganika na kushirikiana katika kuenzi kauli mbiu ya Rais Magufuli ya hapa kazi tuu ili wawe kitu kimoja hali ambayo italeta chachu na kuaminika kwa Wanachama na hivyo bila ya kuwa na makundi yeyote baina yao.

No comments:

Powered by Blogger.