JESHI LA POLISI NCHINI LATAHADHARISHWA KUTEKWA KWA MWANAHABARI SALMA SAID.
Mwandishi wa habari Bi. Salma
Said,anaedaiwa kutekwa na watu siojulikana kwenye uwanja wa Mwalimu Julias
Nyerere
Baraza la habari nchini Tanzania MCT
kwa kushirikiana na taasisi nyingine nne zimetoa siku mbili kuanzia leo kwa
jeshi la polisi nchini kuhakikisha linafanya uchunguzi na kufanikiwa kumpata
mwandishi wa habari Bi. Salma Said anayedaiwa kutekwa.
Wakitoa tamko la pamoja, Katibu
Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga, Mkurugenzi wa mtandao wa watetezi wa haki
za binadamu THRDC Bw. Onesmo Olengurumwa pamoja na mwenyekiti wa jukwaa la
wahariri TEF Bw. Theophil Makunga wamesema kitendo hicho kinakwenda kinyume na
misingi ya haki za binadamu.
Viongozi hao wamesema kuwa Licha ya
kitendo hicho pia kuminya uhuru wa wanahabari na haki ya kupata habari, lakini
pia kinajenga hofu kubwa miongoni mwa wanahabari na jamii kwa ujumla.
Aidha vyombo hivyo vimetaka vyombo vya
usalama kuhakikisha vitisho vyote dhidi ya wanahabari na watetezi wa haki za
binadamu visiwani Zanzibar vinakomeshwa na kuwaacha wawe huru kufanya kazi zao
katika kipindi cha uchaguzi wa marudio.
Hivi karibuni Bi. Salma amekuwa akitoa
taarifa mbalimbali za hali ya kisiasa visiwani Zanzibar kupitia Idhaa ya
Kiswahili ya Ujerumani na mitandao ya kijamii ambapo alisema kuwa kuandika
kwake habari hizo alikuwa akipata vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana na hapo
jana katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ilisemekana
mwandishi huyo alitekwa na watu wasiojulikana.
No comments: