LIVE STREAM ADS

Header Ads

LOLLI POP ATAKA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI NCHINI WAOMBEWE.

Mwimbaji na Mtayarishaji wa Muziki wa Injili nchini Goodluck Gozbert maarufu kwa jina la Lolli Pop, amewahimiza Wapenzi wa Muziki wa Injili nchini kuendelea kuwaombea waimbaji wa muziki huo ili waendelee kufanya kazi zuri na bora zaidi.

"Mashabiki wasichoke kutuombea na kutuSupport. Sisi tupo kwa ajili yao na katika kuhakikisha tunainua huduma hii ya uimbaji". Alisema Mwimbaji huo anaetamba na nyimbo kama Ipo Siku, Acha Waambiane, Nimesamehe, Pendo Langu pamoja na Suprise, wakati akizungumza na BMG.

Mbali na Muziki wa injili, pia Lolli Pop amejizolea umaarufu mkubwa nchini kutokana na uwezo wake wa kuandaa muziki wa aina mbalimbali ikiwemo Bongo Fleva ambapo shughuli zake nyingi za sanaa anazifanyia Jijini Mwanza kupitia Studio yake iitwayo Min Sound Studio.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.

No comments:

Powered by Blogger.